Wednesday, April 27, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UONGOZI WA BARAZA LA TAWLA NA UONGOZI WA SKAUT LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa lengo la kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya Chama hicho.
Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Wawakilishi na Wanachama wa Chama cha SKAUT Nchini wakati ujumbe wa wawakilishi hao ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa ajili ya kumuelezea Makamu wa Rais shuhuli zao za kiutendaji hasa katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa Mtoto wa kike.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Katibu Mkuu Kiongozi Baolozi Peter Kijazi Baada ya kuapishwa Makatibu wa Mikoa leo April 27,2016 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR).
---
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi kubwa ya Chama Cha Skauti wa Kike nchini hivi sasa ni kuhakikisha kinarejesha heshima ya mwanamke katika jamii.

Samia ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika ofisi kwake Ikulu kwa ajili ya kuelezea shughuli zao katika kusaidia watoto wa kike waweze kujitambua na hatimaye kulitumikia Taifa.

Alisema pamoja na chama hicho kinafundisha kujenga ujasiri na kuwa huru kwa mtoto wa kike lakini kuna haja ya kukumbushana umuhimu wa kuzingatia mila na desturi nzuri zilizopo katika matendo yao ili kurejesha heshima ya mwanamke.

"Sasa hivi utakuta binti kavaa kipanti kinambana hasa, anazunguka barabarani huku na kule, mwenyewe anajiona yuko sawa...hicho ni kinyume kabisa na maadili yetu, mila na desturi zetu za kiafrika tumeziacha kabisa." alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisema katika enzi hizi za utandawazi kumekuwa na urushwaji wa mambo yasiyo na maadili katika mitandao jambo ambalo mtoto wa kike anaweza kuutumia uhuru huo kwa kufanya mambo kinyume na mila na desturi.

Alisema pamoja na kwamba Tanzania inapingwa na mataifa makubwa kwa kupitisha sheria ya makosa ya mtandao lakini bado chama hicho kina kazi kubwa ya kusaidia jitihada za serikali katika kulea watoto wa kike kimaadili. 

"Nyinyi Girl Guide mna hiyo kazi ya kusaidia kuwalea watoto wa kike waliojengeka vizuri kimaadili na wanazingatia mila na desturi," alidokeza Samia

Makamu wa Rais alikitaka chama hicho pia kuandaa miradi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo bora mashuleni kulingana na mahitaji ya watoto wa kike na hivyo kuwawezesha kuhudhuria masomo siku zote bila kukosa kama ilivyo kwa wavulana.

Mwenyekiti wa chama hicho, Matilda Balawa alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kuwa mwanachama na kupongeza utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu