Thursday, April 21, 2016

MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WANAFUNZI NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING - CHINA

Picha ya Pamoja
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho akizungumza jambo mbele ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu(hawapo pichani), katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China
Mmoja wa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambae pia ni Mwanafunzi,akizungumza jambo mbele ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu(hawapo pichani), katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China,ambapo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho alikuwa mgeni rasmi .
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 20th April 2016 alikutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China.

Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kwamba wako tayari kurudi nyumbani na kutumia elimu zao katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa.

Katika mazungumzo na Wanachama hao, Mhe Kikwete amewakumbusha jukumu kubwa lililo mbele yao la kujenga Chama na kulijenga Taifa la Tanzania, katika hotuba yake ameeleza kuwa China imefanya Mapinduzi makubwa katika maendeleo na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hiyo, hivyo kuwataka kujifunza na kuchukua maarifa ya China na kuyatumia wakirudi nchini ili kufanikisha Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Mheshimiwa Kikwete na Ujumbe wake wanatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou hapo kesho na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa CCP na Rais wa Serikali ya watu wa China Mhe Xi Jinping, pamoja na kufanya mazungumzo muhimu na Viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China {CCP} katika jimbo hilo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu