Tuesday, April 5, 2016

MWENYEKITI WA MTAA AWEKWA KITI MOTO KWA KUGHUSHI MUKHTASARI

 Na Woinde Shizza, Arusha

Kamati ya nidhamu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Ngarenaro jijini Arusha imemweka “kitimoto” mwenyekiti wa mtaawa mita 200,Winstone Laiser kwa madai ya kughushi mukhtasari wa kikao cha kamati ya utendaji jambo ambalo ni kinyume na sheria za chama hicho.

Kikao hicho ni kilekinachodaiwa kuketi mnamo Oktoba 6 mwaka jana ambacho kilihudhuriwa na wajumbewatano huku kikiwa na ajenda ya kujadili ajenda ya kumtambua aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kasulu, Dahni Makanga kwamba ni mkazi wa eneohilo.

Hatua hiyo imefuatiamara baada ya baadhi ya wajumbe wanaodaiwa kuhudhuria kikao hicho kufikisha malalamikiayao mbele ya uongozi wa chama hicho na kulalalmikia kitendo cha majina yaokuandikwa katika mukhtasari huo ingawa hawakushiriki kikao hicho.

Kwa mujibu wa taarifazilizolifikia gazeti hili zimedai kwamba kamati ya nidhamu ya kata ya Ngarenaroilimhoji Laiser juzi kwa lengo la kumpa nafasi kujibu tuhuma za kughushimukhtasari huo .

Taarifa hizo zimedaikwamba baadhi ya wajumbe katika kikao hicho walimbana mwenyekiti huyo kwakutaka kujua kweli wa tuhuma hizo ambapo baadhi yao walionekana kushtushwa nataarifa kwamba mukhtasari huo unatumika kamakielelezo katika mgogoro wa kugombea ardhi ndani ya kata hiyo.

Hatahivyo,kwa mujibu wataarifa ndani ya kikao hicho zimedai kwamba mwenyekiti huyo alijitetea kwambaalirubuniwa na baadhi ya watu huku akiiangukia kamati hiyo ya nidhamu kwa lengola kuiomba msamaha.

Mmoja wa wajumbe ambaoamepinga kitendo cha jina lake kutajwandani ya mukhtasari huo ingawahakushiriki kikao hicho, Peter Lukumay alisema kwamba wanapinga kwa nguvu zotekitendo hicho kwa kuwa wanaweza kuingizwa katika kesi ya jinai.

Alipoulizwa Laiserkuhusu taarifa za kuhojiwa na kamati hiyo alisema kwamba aulizwe aliyetoataarifa hizo huku akisisitiza kwamba atachukua hatua anazozijua endapo taarifahizo zikiandikwa gazetini.

“Wewe nenda kamuulizehuyo aliyekupa taarifa hizo lakini kama ukiandika hizi taarifa mimi nitachukua hatuaninazozijua “alisema na kisha kukata simu Mwenyekiti wa Chadema kata ya Ngarenaro, Steven Urasa alipohojiwa kuhusu taarifa hizo alikirikufanyika kwa kikao hicho huku akisema kwamba anasubiri mapendekezo ya kamatihiyokabla ya kuyawasilisha mbele ya uongozi wa Chadema ngazi ya wilaya.

Hata hivyo, mwenyekiti waChadema wilaya ya Arusha, Dereck Magoma alikiri
uongozi wake kupokea taarifahizo na kusisitiza kwamba anasubiri maamuzi ya kikao kilichoketi kujadili sualahilo kabla hajatangazahatua zilizochukuliwa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu