Mafundi wa kampuni ya Estim Construction wakiendelea na Ujenzi wa barabara ya Mwenge –Morocco KM 4.3 ambayo ni sehemu ya Barabara ya Morocco –Mwenge-Tegeta.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kazi ya ujenzi wa mifereji pembezoni mwa Barabara ya Morocco-Mwenge inavyoendelea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng.Patric Mfugale kuhusu kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Morocco-Mwenge KM 4.3.
--
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa mkandarasi ESTIM Construction anayejenga barabara ya Bagamoyo, Sehemu ya Morroco-Mwenge kilomita 4.3 kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.

Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo, Prof. Mbarawa amesema baada ya wiki mbili barabara hiyo itafunguliwa kwa ajili ya matumizi ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka katikati ya jijini.

“Hakikisheni barabara hii inakamilika ndani ya wiki mbili, ili msongamano wa magari yanatoingia na kutoka katika ya jiji upungue, na hivyo kuiunganisha vizuri barabara hii na ile ya Mwenge-Tegeta”. Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha amewataka waananchi na madereva wanaotumia barabara hiyo kulinda mazingira kwa kuepuka vitendo vya kumwaga mafuta kwenye barabara hiyo na kutupa takataka zinazosababisha mifereji iliyo pembezoni mwa barabara kuzipa na kuharibu barabara hiyo.

“Nawataka watumiaji wa barabara, kuzingatia matumizi sahihi ya barabara, tunawekeza fedha nyingi katika ujenzi wa barabara mijini ili kuondoa msongamano hivyo zingatieni matumizi sahihi ya barabara ili zidumu kwa muda mrefu”. Amesema Prof. Mbarawa.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwa ili kupunguza msongamano ujenzi wa barabara hiyo umelazimika kuweka sehemu maalum za watembea kwa miguu kutokana na wingi wa watumiaji wa barabara hiyo katika sehemu hiyo na kupanua maingilio ya barabara ili kurahisisha magari kutoka na kuingia katika barabara hiyo.

Eng. Mfugale amesema zaidi ya magari 15,000 yanakadiriwa kuwa yatapita katika barabara itakapokamilikana hivyo kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo katika eneo hilo.

Takribani shilingi bilioni 4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo na hivyo kuiunganisha barabara ya Mwenge-Morroco na ile ya Mwenge-Tegeta.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: