Monday, April 11, 2016

TRAVELSTART YATUNUKIWA TUZO YA WAKALA BORA KWA MWAKA 2016 NA WORLD TRAVEL AWARDS

 Meneja Mkurugenzi wa Travelstart Tanzania Abbas Rajani (kati) akipokea tuzo ya WTA ya 'Tanzania's Leading Travel Agency 2016', kulia ni Chris Frost, Makamu Rais wa World Travel Awards (WTA).
---
Kampuni ya Travelstart Tanzania imefanikiwa kupata tuzo ya Wakala Bora wa Ndege (travel agency) nchini ya World Travel Awards (WTA) katika hafla maalum iliyofanyika Jumamosi iliyopita pale Diamonds La Gemma, dell’Est kisiwani Zanzibar.

Kila mwaka WTA hufanya hafla maalum katika kanda mbalimbali ili kutambua na kusheherekea mafanikio ya binafsi na pamoja ya washindi wake. Tuzo za WTA zinasifika sana katika sekta ya usafiri na utalii huku ufahari wake ukilinganishwa na tuzo za “Oscars” kwa tasnia ya filamu.

Washindani wa tuzo hizi huchaguliwa na wataalamu wa kimataifa katika sekta husika ambapo kwa mwaka huu Travelstart Tanzania imeshinda kwa mara ya kwanza ikiwa kama kampuni pekee ya wakala inayotumia mtandao wa “internet”.

Bwana Abbas Rajani, Meneja Mkurugenzi wa Travelstart Tanzania, alikuwa na haya ya kusema: “Tumefurahi kwa heshima hii tuliyotunukiwa na World Travel Awards. Shukrani za kipekee ziwaendee wapiga kura waliotuwezesha kushinda tuzo hii. Tunajivunia uwezo wetu wa kuwapa wateja zetu bei nafuu kuliko wengine wote. Pamoja na kuwa kampuni changa na endelevu, Travelstart ni kiongozi katika unafuu, chagua na mitindo mbalimbali bila kusahau utoaji wa huduma bora zaidi.

“Tutaendelea kuleta mabadiliko endelevu katika tasnia hii ili kuondoa ugumu na kero zinazojitokeza kwa wateja wetu. Wakati huo huo Travelstart itaendelea kukua na kuboresha huduma kulingana na mahitaji ya wasafiri pamoja na sekta hii changamfu la Tanzania”

Kampuni ya Travelstart Tanzania inapenda kuwashukuru wafanyakazi, washirika na wateja wake wote waliokuwa nasi katika safari hii hadi kufikia hatua hii kubwa. Tunaahidi kuendelea kuwapa kile kilicho bora zaidi katika sekta ya usafiri.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu