*Kijana mmojawapo atawezeshwa kwa vitendea kazi katika warsha hiyo

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, imeandaa warsha maalumu ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 - 24 katika mkoa wa Dar es Saalam na kuwaalika vijana kujitokeza kupata mafunzo ya namna ya kuendesha biashara zao.

Warsha hiyo ya mafunzo itafanyika Jumanne ya tarehe 19/04/2016, katika ukumbi wa Urafiki Social hall ulioko shekilango jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 2 asubuhi.

Katika Warsha hiyo kijana mmoja atakayeweza kuelezea na kuwakilisha changamoto anazozipata katika biashara aliyonayo mbele ya jopo la washauri na vijana wenzake ataweza kupata bahati ya kupatiwa vifaa vya kazi kwa ajili ya kuendeleza biashara yake.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja huduma za jamii wa Airtel Bi.Hawa Bayumi alisema, "Airtel Fursa imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia na kuwawezesha vijana wengi nchini kupata elimu na pia kuwapatia misaada wa vitendea kazi itakayowawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi"

Mpaka sasa tumeshafanya semina kama hizi katika mikoa ya Dar es Saalam, Arusha, Mbeya, Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mtwara Dodoma na Iringa na kuwawezesha vijana zaidi ya 3700 kupata mafunzo hayo muhimu ikiwemo usimamizi wa mtaji, mbinu za masoko, kuzitambua fursa na ujuzi wa kibiashara, namna ya kuendesha biashara na kuweka mahesabu , jinsi ya kufungua akaunti benki na nyingine nyingi"

Aliongeza kwa kusema "Kwa wakazi na vijana wa Dar Es Salaam hii ni nafasi ya kipekee kwa vijana wa Dar es Salaam kwani mafunzo haya yanarudi kwa mara ya pili jijini Dar, tunatoa wito wajitokeze kwa wingi kupata mafunzo haya bure bila gharama yoyote kupitia wataalamu wetu mahiri wenye ujuzi katika maswala ya biashara na ujasiriamali"

Tunaamini vijana wengi watatoka katika mafunzo haya wakiwa wamewezeshwa kuwa na mtazamo chanya lakini zaidi wakiwa na mbinu za kuendesha biashara zao kwa mafanikio zaidi.

Airtel kupitia Airtel Fursa itaendelea kutoa warsha kama hizi maeneo mbalimbali hapa nchini na kuweza kufikia vijana wengi zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: