Tuesday, April 12, 2016

VITAMBULISHO VYA TAIFA VINAENDELEA KUTOLEWA ZANZIBAR

 Mkuu wa Brigedi Nd.Sharif Sheikh Othman akipokea kitambulisho chake toka kwa mfanyakazi wa NIDA ofisi ya Zanzibar; hayupo pichani.

Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inaendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu pamoja na kugawa Vitambulisho kwa Wananchi wa Zanzibar kwa makundi tofauti walikokamilisha taratibu zote msingi za usajili na Utambuzi

Kwa sasa NIDA inaendelea na zoezi la Ugawaji vitambulisho kwa Askari na Wanajeshi Kisiwani Pemba. Zaidi ya vitambulisho 1,063 vimegawanywa. Askari hao na Wanajeshi wameonyesha kufurahishwa sana na Hatua ya Mamlaka ya kukamilisha zoezi la Usajili na kuwapatia Vitambulisho vya uraia.

Zoezi la utoaji vitambulisho liliendeshwa katika Mikoa yote ya Pemba katika vituo na makambi ya vikosi hivyo, JWTZ Alkhamis Camp, Polisi Wete, Polisi Micheweni, Polisi Mkoani na Polisi Chake Chake.

Tayari zoezi kama hili lilifanyika Unguja kwa vikosi vya ulinzi na usalama; na hatua za usajili zinaendelea kwa wale ambao hawakushiriki zoezi la awali kupitia ofisi zetu za Wilaya.

NIDA imeendelea na zoezi la utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi, Wafanyakazi wa Idara na Taasisi mbali mbali za za SMZ na SMT pamoja na kufanya usajili mpya kwa wananchi ambao wamekuwa wakitimiza umri wa miaka 18 na wananchi ambao hawakushiriki zoezi la awali la usajili wa jumla.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu