Mwanamuziki mahiri  wa Rnb hapa nchini  , Bernard Michael Paul, maarufu kama ‘Ben Pol’ akitoa burudani  kwa maelfu ya wakazi wa Dar es salaam waliohudhuria maadhimisho ya miaka mitano ya Tamasha la Nyama choma 2016, ambapo Tigo ilimdhamini kutumbuiza katika tamasha hilo , mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.

BEN POL akicheza na mashabiki zake jukwaani wakati wa tamasha la nyama choma katika viwanja vya leaders Jijini Dar es Salaam.
Mashabikiwa muziki wa bongo fleva wakishangilia wakati Benpol anatumbuiza kibao chake cha MOYO MASHINE 

Benpol akihojiwa na mtangazaji wa Clouds fm Askofu Tza baada ya kutumbuiza katika tamasha la Nyama choma mapema jana katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.

Baadhi ya mawakala wa tigo waliokuwepo katika viwanja  vya Leaders kutoa msaada na huduma mbali mbali toka tigo ikiwemo huduma za intaneti ya kasi ya Tigo 4G LTE
Wakala wa tigo akisajili laini ya mteja katika tamasha la Nyama choma mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.


Mtangazaji wa Choice fm na mshindi wa Bigbrother 2014 Idris sultan akifurahi jambo na Mcheza kikapu wa kimataifa Hasheem Thabit wakati wa Tamasha la Nyama Choma lililofanyika mapema jana usiku katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaam.
Msanii mahiri wa Bongo fleva Vanessa Mdee akiongea jambo na mmoja wa shabiki zake katika viwanja  vya Leaders Jijini Dar es salaam
Mabanda ya tigo yaliyokuwepo uwanjani katika kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa tigo  waliofika katika tamasha la Nyama Choma 

Mmoja wa wapishi wa nyama akichoma nyama wakati wa tamasha la Nyama Choma mapema jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Wadau wakiendelea kufurahia muziki na kula nyama choma katika tamasha liliofanyika mapema jana


Mmoja wa wakala wa Tigo akimsaidia mteja  kufungua intaneti ya tigo katika simu yake katika tamasha la Nyama Choma .liliofanyika mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam,

Maelfu ya wakazi waliofika katika tamasha wakifurahia muziki toka kwa wasanii mbali mbali waliotumbuiza jukwaani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: