Tuesday, May 31, 2016

CLUB 777 YAENDELEA KUWA KIVUTIO KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR

Dj Dokta Michael Saduka akifanya yake ndani ya Club Triple 7, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Wapenzi wa burudani wakivinjari ndani ya Club 777.
Maua.
Show Love.
Unapozungumzia Club bora jijini Dar es salaam huwezi kuiacha Club Triple 7 iliyopo maeneo Kawe/Mikocheni ni sehemu ambayo mastaa wengi na watu mbali mbali hupendelea kufika kwa ajili ya burudani nzuri ya muziki inayopatikana hapo.

Siku za jumatano huwa ni usiku wa Karaoke ambapo watu hufika hapo kwa ajili ya kuimba nyimbo mbali mbali wazipendazo, lakini balaa zaidi huwa ni siku za ijumaa na jumamosi ambapo huwa ni siku za Club kwa ajili ya watu kula bata na kupata mziki mzuri.

Michael Saduka si jina geni miongoni mwa masikio ya wasikilizaji wa radio hapa nchini, ni mtangazaji aliyepitia kituo cha Times fm, Magic fm na E fm ndie Dj wa Club Triple 7, nilishangaa kumuona Triple 7 kwa jinsi anavyowarusha, watu mbali mbali ambao hufika hapo.

Nikapata bahati ya kuzungumza na watu mbali mbali sababu ya kwanini hupenda kufika Triple 7 licha ya Dar kuwa na Club mbali mbali wengi wamesema ni huduma nzuri za vyakula na vinywaji ila funga kazi ni burudani ya Mziki kutoka kwa Michael Saduka aka Dj Micklove

"Huyu jamaa bwana anajua nini anachofanya ana selection nzuri ya music, ana mix vizuri, anapiga ladha nzuri ambapo kweli una feel kuwa uko club, Mimi nitaenda club zote lakini Triple 7 lazima nifike" Alisema mmoja wa shabiki alikamatwa na Camera yetu.

Na kwa upande wa Michael Saduka alipoulizwa anajisikiaje kuwapa burudani wakazi wa jiji la Dar es salaam na kuchizika alisema "Mimi nahisi faraja sana kwa maana muziki ninaujua kwa muda mrefu na ladha yangu ya muziki iko tofauti sana na ma dj wengi na kuna wageni mbali mbali hutembelea club yetu kutoka mataifa mbali mbali na nimeshapata mialiko mingi ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuburudisha, am so proud to be at Triple 7, wategemee mambo makubwa" Alimalizia kusema Michael Saduka aka Dj Micklove.

Hayo ndio mambo ya Triple 7, kama hujawahi kufika hebu fika weekend ukajionee burudani za uhakika.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu