Dr. Hamisi Kigwangalla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameutangazia umma wa watanzania kuwa ameshusha kiwango cha kodi inayotozwa kwenye mshahara wa wafanyakazi wa ngazi ya chini (lower bracket) kutoka 11% mpaka 9%. Hili ni punguzo la kihistoria.

Najua malengo ya kufanya hivi ni kukidhi haja ya watumishi ya muda mrefu kuwa kiwango cha kodi kishuke kiwe 'single digit', pia kupunguza mzigo wa kodi kwa watumishi na hivyo kuwaongezea kipato chao. Pia ameweka msisitizo kwenye azma yake ya kushusha kiwango cha mshahara wa waliokuwa wanalipwa mishahara mikubwa na kuhakikisha haizidi 15mn - lengo likiwa ni kupunguza 'gap' kati ya walionacho na wasionacho kwenye nchi.

Ukimsikia Rais Magufuli anazungumzia mambo ya kuleta usawa nchini utajua wazi kabisa kuwa 'maneno yake yanatoka kwenye special corner ya moyo wake', maana anayazungumza kwa 'passion' ya hali ya juu sana kiukweli. Kwenye hili, ninamuahidi, kwa dhati kabisa, kumsaidia kutimiza hayo malengo yake kwa nguvu zangu zote, na kwa 'passion' na kasi kama ya kwake. Maana ni katika mambo ninayoyaamini na yaliyonifanya niingie Bungeni kwenye utumishi kwa wananchi, na 'passion' hiyo inatoka moyoni mwangu kabisa. Wakati natangaza nia ya kuomba nipewe ticket ya CCM kuwa mgombea wake wa uRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliwahi kusema kuwa 'kizazi chetu cha viongozi kisikubali tuwe na matabaka ya aina mbaya kabisa kwenye nchi yetu: kwamba, tuna kundi moja la watu wengi wanaoamka kila siku asubuhi na kutembea maili 10 kusaka mlo wa siku hiyo, huku tuna kundi lingine linalotafuta walau muda wa kutembea maili 10 ili kukata vitambi vyao!'

Somo kubwa la kujifunza hapa ni kwamba, mfanyakazi hana namna ya kukwepa kodi ya serikali ya PAYE, maana serikali anachukua kodi yake kwanza kabla mfanyakazi hajalipwa mshahara. Tofauti na wafanyabiashara, ambao wanazalisha, kisha wanaanza mambo ya makadirio ya kodi ya serikali. Niliwahi kusoma kitabu cha Robert Kiyosaki, Rich Dad - Poor Dad, anayesema kuwa 'watu wajanja hawawezi kukubali kuajiriwa, maana hawawezi kuwa tayari kukubali kukatwa kiasi kikubwa cha pesa kama kodi, wajanja hujiajiri wenyewe kwa kuwekeza na kuzungusha mitaji kutafuta faida kisha kutafuta kila namna ya kukwepa kodi ya serikali, na hivyo kundi hili la pili huishi maisha ya raha kwa kuwa lina uhakika wa kutajirika.'

Kwa vijana wa nchi yetu wanaohangaika kutafuta ajira siku hata siku wana la kujifunza hapa. Kama wanataka mali, watayapata shambani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: