Monday, May 9, 2016

FIRST NATIONAL BANK YAFUNGUA TAWI MWANZA

Mkuu wa Biashara FNB Tanzania, Francois Botha akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella jinzsi mashine ya kisasa ya kuolea fedha inavyofanya kazi baada ya mkuu wa mkoa kuzindua huduma za benki hiyo jijini Mwanza.
---
Benki ya First National Bank Tanzania (FNB) imeendelea kupanua wigo kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la Rock City Mall jijini Mwanza leo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Francois Botha alisema uzinduzi wa tawi la FNB Mwanza umelenga kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za kibenki na za kifedha katika mkoa huo.

“Uzinduzi wa tawi la Mwanza ni sehemu ya uwekezaji endelevu na mkakati wa kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia tumezingatia ukuaji wa haraka wa mkoa wa Mwanzaambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.”

Botha alisema tawi Mwanza ni la tisa miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mtandao wa matawi ili kuyafikia maeneo yote nchini.

“ First National Bank daima tunafikiri njia mbalimbali za ambazo tunaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Mwanza litatoa ufumbuzi wa kina kwa wateja wanao ishi Mwanza na maeneo jirani yenye biashara inayokua kwa kasi” Botha alisema.

Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishi jijini Mwanza na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi,” alisema Botha.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema mkoa wa Mwanza una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji mkubwa wa sekta mbalimbali za kiuchumii karibuni ni ishara kuwa Mwanza inakua kwa kasi.

"Tunakaribisha uwepo wa FNB na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha huduma zenu hapa na mikoa mengine," alisema Mkuu wa Mkoa.

Alisema mbali na mkoa wa Mwanza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi bali pia inazalisha mali nyingi na ina utajiri mkubwa wa rasilimali. “Tunatarajia kuwa mtatoa mchango mkubwa katika utoaji huduma za kifedha mkoani Mwanza kupitia huduma zenu mbalimbali kwa kutumia ubunifu na utaalamu wenu,” Mongella alisema.

Tawi hilo lililofunguliwa kwenye jingo jipya la Rock City Mall litatoa huduma za kawaida za kibenki pamoja na huduma za dijitali kwa masaa 24 ili mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu