Bi. Esther Chiombola akionyesha uyoga ambao uko tayari kuvunwa. Uyoga huo unalimwa na kikundi cha Tunza Women Group cha Bunju jijini Dar es Salaam kwa ufadhili wa mradi wa Green Voices (Makala na Picha zimeandaliwa na www.brotherdanny.com).
Bi. Sauda Issa miaka 70 (kushoto) mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam akipokea zawadi ya kitabu maalum kinachozungumzia kilimo cha uyoga kutoka kwa Bi. Esther Chiombola ambaye ni Ofisa Kilimo Msaidizi Mwandamizi wa Manispaa ya Kinondoni.
Mratibu wa vikundi vya kilimo cha uyoga Bunju na Boko, Magdalena Bukuku (katikati) akiteta jambo na mratibu wa green Voices nchini Bi. Secelela Balisidya wakati wa uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Green Voices. Wengine pichani kutoka kushoto ni Bi. Lucresia Tarimo aliyemwakilisha Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Kinondoni, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Seif Stambuli, na Ofisa Kilimo Kata ya Bunju, Rhoda Mruttu. 
Bi. Sophia Chove, mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa uyoga Bunju, akitoa maelekezo kwa watu mbalimbali kuhusu namna ya uchanganyaji wa vimeng’enyo vya kuoteshea na kukuzia uyoga. 
Mchanganyiko maalum wa vimeng’enyo vinavyotumika katika kilimo cha uyoga. 
Uyoga ukiwa unaoteshwa katika eneo maalum kwa kufunikwa kaniki. 
Mchuzi mzito wa uyoga ulioandaliwa kwa ajili ya chakula cha mchana. Uyoga huo umevunwa katika mradi wa kikundi cha akinamama wa Bunju chini ya ufadhili wa Green Voices. 
Wageni waalikwa wakishiriki chakula cha mchana ambacho mboga kuu ilikuwa uyoga. 
  Akinamama sita, ambao ni sehemu ya akinamama 15 ambao wanatekeleza mradi wa Green Voices baada ya kupatiwa mafunzo nchini Hispania mwanzoni mwa mwaka huu. Kutoka kushoto ni Siddy Abubakar Mgumia, Farida Hamisi, Tukuswiga Mwaisumbe, Secelela Balisidya, Magdalena Bukuku na Judica Losai.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: