Thursday, May 19, 2016

LAFARGE YAZINDUA SARUJI YA WAASHI TEMBO FUNDI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Ilse Boshoff na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa kapuni hiyo Allan Chonjo (kulia) wakizindua chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Fundi” ambayo ni mahususi kwa ajili ya uashi leo kwenye kiwanda cha Saruji cha Tembo Cement jijini Mbeya (Picha: Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Ilse Boshoff (katikati) na Emily Sindato (kulia), Mkuu wa Ufundi wa kiwanda hicho wakizindua chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Fundi” ambayo ni mahususi kwa ajili ya uashi leo kwenye kiwanda cha Saruji cha Tembo Cement jijini Mbeya (Picha: Mpiga Picha Wetu)
---
Kampuni ya Saruji Lafarge Tanzania imezindua saruji ya kwanza maalumu kwa matumizi ya uashi. Saruji hii inayojulikana kama Tembo Fundi itawapa wajenzi chaguo bora kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni pamoja na kupiga plasta ukuta, kusakafia, kujengea tofali na kupangilia marumaru. Saruji hiyo iliyotengenezwa maalum kwa kazi ya uashi wa kuta za nje na ndani ina ubora katika kufanya kazi, nguvu kwenye ugundishaji inashika vizuri na ina umaliziaji bora wenye kuleta matokeo yaliyo bora zaidi kwenye kujenga tofali, uzio, marumaru na sakafu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Ilse Boshoff, alisema wakati wa uzinduzi leo kwamba Tembo Fundi imeundwa mahususi kwa ajili ya kazi za uashi na kuwapa wajenzi utendaji bora wa kazi na thamani ya fedha.

“Ikiwa imetengenezwa kutokana na uzoefu na utaalamu wa Lafarge kimataifa katika kuzalisha saruji, Tembo Fundi ni rahisi kutumia katika kupiga plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla ambayo itamchukua muashi muda mrefu katika kusawazisha ukuta.

Alisema faida nyingine muhimu katika matumizi ya Tembo Fundi ni unafuu katika gharama kutokana na mfuko mmoja wa Tembo Fundi kutumika eneo pana zaidi ukilinganisha na mfuko wa saruji ya matumizi ya jumla. Kutokana ya kwamba inafanya kazi vizuri na uimara wake kudumu kwa muda mrefu Tembo Fundi itawasaidia wajenzi kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo alisema daima Lafarge imekuwa ikiwasikiliza wateja wake. Tembo Fundi ndio suluhisho la mahitaji ya saruji yenye ubora kwani inatumia maji kidogo, inadumu, haipati nyufa na ina uwezo wa kujenga eneo pana zaidi na kuufanya ukuta wako ung’ae zaidi.

“Tembo Fundi inapatikana katika ujazo wa kilogramu 50 na ni ubunifu wetu katika kurahisisha kazi za uashi. Lafarge imewekeza sana katika utafiti uliopelekea uvumbuzi wa saruji kama hii ambayo inapendwa na wajenzi katika masoko mbalimbali kimataifa. Hii ni moja ya dhima zetu za kuhakikisha tunawapa wajenzi sulhisho maalumu katika kazi zao. Tembo Fundi itasambazwa katika maduka yetu yote ya jumla na rejareja pamoja na kwenye kontena zetu za usambazaji.

Hivi sasa kwenye soko la saruji hakuna saruji iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya uashi jambo ambalo linawalazimisha watumiaji kutumia saruji ya matumizi ya jumla kwa ajili ya kazi za uashi na kupelekea ongezeko la gharama za ujenzi na kukosa matokeo mazuri katika ujenzi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu