Tuesday, May 3, 2016

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI APOKEA MSAADA WA MADAWATI KUTOKA LAPF

Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa kamati ya Huduma, uchumi na elimu Diwani Tungaraza akipokea madawati kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa LAPF.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi leo hii amepokea madawati 124 kutoka kwa mfuko wa jamii wa LAPF kama mchango wao kupunguza kero ya madawati kwa shule za manispaa ya Kinondoni. Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika leo mbele ya ofisi ya mkururugenzi wa manispaa ya Kinondoni.

Akiongea wakati akikabidhi madawati hayo mkurugenzi wa Mawasiliano James Mlowe amesema wameteua manispaa hii kuwapa msaada wa madawati kwa kuwa wafanyakazi wa wilaya ya Kinondoni wamekuwa niwafanyakazi wanaoongoza kuleta michango kwa wakati ukilinganisha na halmashauri zingine.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu