Kampuni ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa bidhaa za DStv nchini usiku wa Mei 26 wameweza kujumuika kwa pamoja katika kusheherekea siku ya Afrika kwa kukutana na wadau wake Jijini Dar es Salaam na kufurahia paamoja fahari ya Afrika.
Wadau hao ni pamoja na wanahabari, Waendesha vipindi vya televisheni na radio, wasanii na baadhi ya wateja ambao walijumuika kwa pamoja usiku maalum ambao pia walipata kula na kunywa pamoja na kubadilishana mwazo.
Awali wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo maalum, Meneja Uhusiano na Masoko wa MultiAChoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu alieleza kuwa, MultiChoice wanajisikia fahari katika ushiriki wao wa kuleta mabadiliko na maendeleo tangu kuanzishwa hapa Barani Afrika miaka 20 iliyopit huku ldngo kuu ni kuwa na maudhui ya kila siku ya kiafrika.
Aidha, Bi. Furaha Sumalu alibainisha kuwa, kwa kuthamini Afrika, hata chaneli wameweka zinazolenga Afrika zikiwemo: Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East ambapo ndani ya chaneli hizo zimekuwa na mtazamo tofauti kuhusu Afrika hivyo watanzania na waafrika kwa ujumla ni wakati wa kuchangamkia bidhaa bora za DSTV ilikufurahia uhondo huo wa Kiafrika na mambo mbalimbali yanayotokea ndani ya Afrika nan je ya Afrika.
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:



Msanii Uwoya (kulia) akiwa katika red carpet..

Wadau wa DSTV, wakifuatilia tukio hilo


Burudani za ngoma zikiendelea



Baadhi ya watendaji wakuu wa DSTV wakitambulishwa






Muda wa 'msosi' ulikuwa kama hivyo pichani.








Burudani zilipamba moto zaidi..



Msanii Shilole 'Shishi bebi' akitangaza bahati nasibu ya mshindi w dikoda ya DSTV Exp

Mshiriki wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother III, Latoya Lyakurya, akipokea zawadi ya dikoda ya DSTV.

Mwanablog ya Fullshangwe, John Bukuku akishangilia baada ya kutangaza kushinda zawadi ya dikoda ya DSTV

Mwanablog ya Fullshangwe, John Bukuku akipokea dikoda yake

Mke wa msanii Sheta, Leila Yusuph 'Mama Quila' akisoma jina la mshindi


Mmiliki wa mtandao wa Wananchi, Bw. William Malecela 'Lemutuz' akitangaza jina la mshindi



Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo akikabidhi zawadi

Baadhi ya staff wa DSTV

Othuman Michuzi wa blog ya Mtaa kwa Mtaa akipokea zawadi yake wakati wa hafla hiyo ya usiku wa Afrika na DSTV.



Wadau wakisakata rhumba.

Wasanii wa kundi la NIMUJO Edutaiment wakicheza ngoma za makabila mbalimbali wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Toa Maoni Yako:
0 comments: