Friday, May 13, 2016

UPDATES: MSIBA WA MTOTO WA ANKAL, MWILI KUWASILI LEO IJUMAA, MAZISHI KESHO JUMAMOSI SAA 10 MAKABURI YA KISUTU, DAR ES SALAAM

Assalaam Aleikhum,
Updates za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18),  aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini:

Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa saba mchana kwa  ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa  ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban). Mwili wa kijana wetu utapokelewa  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi saa 10  alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu  za kuandaa mazishi zitaanza  saa 4 asubuhi siku hiyo hiyo ya Jumamosi, nyumbani  kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.

NAMNA YA KUFIKA MSIBANI

Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa "Twiga Cement",  hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.


Innalillah wa inna ilayhi raajiun
-AMIN.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu