Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akiwasisitiza jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akimweleza jambo Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Bw. Frank Nkya (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kulia)akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angella Kairuki (kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa CCM Jimbo la Mtama akiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge mwenzie wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiwa ameongozana na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Eng. Hamad Masauni wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.

Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge akiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.

Mbunge wa CCM Jimbo la Pangani, Mhe. Jumaa Aweso (kulia) akiwa ameongozana na Mbunge mwenzie wakiingia ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: