Ubalozi wa Denmark nchini kwa kushirikiana na shirika la Marie Stopes Tanzania – MST, Femina Hip; Msichana Initiative; pamoja na wizara ya afya, ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto, wameandaa kongamano kuhusu afya, haki na uwezeshaji wa wanawake litakalofanyika kesho Alhamis May 05, 2016.

Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya maandalizi ya kongamano la kimataifa ambalo mwaka huu litafanyika mjini Copenhagen, Denmark baadaye mwezi huu, litafanyika kwenye Makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam; mada kuu ikiwa ni kwa jinsi gani Tanzania itaweza kufikia malengo endelevu ya milenia kwa wanawake na wasichana ifikapo mwaka 2030.

Kongamano la Copenhagen litakalofanyika kuanzia May 16 hadi 19 mwezi huu, ni kongamano kubwa zaidi la kimataifa linalolenga masuala ya afya, haki, usalama na uwezeshaji wa wanawake na wasichana. Mada kuu ya mwaka huu itakuwa ni utekelezaji wa Malengo mapya ya maendeleo endelevu – SDGs ambayo yaliwekwa na mkutano mkuu wa umoja wa Mataifa Agosti, 2015.

Lengo la mdahalo wa kesho ni kujadili kwa uwazi jinsi Tanzania itavyoweza kufanikiwa kufikia matarajio ya malengo ya maendele endelevu, yanayohusiana na wanawake na wasichana hususani afya ya uzazi na haki zao katika masuala ya usawa wa kijinsia, elimu, mazingira na uwezeshwaji wa kiuchumi.

Mdahalo huu wa wazi utaongozwa na Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu, pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TACAIDS, Fatma Mrisho; Mkurugenzi mkuu wa Chama cha wanasheria wanawake Tanzania, Tike Mwambipile, na Mkurugenzi wa huduma za afya wa shirika la Marie Stopes Tanzania Mwemezi Ngemera.

Mdahalo huo pia utawesha kubaini vipaumbele vya utekeleza kwa Tanzania kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu yanayohusiana na wanawake na wasichana ili kutambua na kudhamini mchango wao katika jitihada za Tanzania kufikia maendeleo endelevu.

Mdahalo huu pia utaambatana na maaonesho ya shughuli mbalimbali za kuhamasisha afya na haki kwa wanawake na wasichana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: