Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance, Hamida Rashid (kulia) akikabidhi zawadi ya nguo, Mzee Filipo Mchopa (katikati) wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwenye kituo cha wazee wa Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki (kushoto) ni Meneja Operesheni wa AAR, Harold Adamson.
 Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance, Hamida Rashid (kushoto) akimsalimia, Shida Uwesu, mmoja wa wazee wanaohudumiwa na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwa wazee hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Ofisa Madai wa Kampuni ya Bima ya Afya ya AAR, Louisa Mwinchumu (katikati) akimkabidhi msaada wa chakula, Hidaya Othuman, mmoja wa wazee wanaohudumiwa na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwa wazee hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
---
Wafanyakazi wa AAR Insurance Tanzania wametoa msaada wa vyakula, mavazi pamoja na vifaa vya matumizi ya nyumbani kwa kituo cha wazee cha Yombo Kilakala kupitia programu maalum ya kusaidia jamii ijulikanayo kama Jaza Kikapu.

Akiongea kwenye makabidhiano ya msaada huo jijini Dar es salaam leo, Meneja Maendeleo ya Biashara wa AAR, Hamida Rashid amesema kwamba kwa muda wa miaka 17 AAR imekuwa na utamaduni wa kuhamasisha wafanyakazi wake kutumia fursa mbalimbali kujitolea kuisaidia jamii hususani makundi ya watu wenye mahitaji maalum kupitia program ya wafanyakazi kujitolea ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakisaidia watu wenye shida mbalimbali.

“Sisi AAR Insurance tunataka kuhakikisha tunatoa mchango muhimu kwenye mambo yanayoigusa maisha ya watu ikiwa ni kwa wafanyakazi wetu pamoja na jamii nzima. Tunatazamia kuendelea na uhusiano mzuri na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala kwa miaka mingi ijayo.”

Rashid alitaja baadhi ya vitu vilivyotolewa msaada kuwa ni pamoja na nguo pamoja na vyombo vinavyotumika kwenye matumizi ya kila siku majumbani ambavyo vilikusanywa kutoka kwa wafanyakazi wa AAR kupitia kampeni yao ya Jaza Kikapu ambapo wafanyakazi walijitolea kutoa vitu mbalimbali kusaidia wenye shida.

Akizungumzia msaada huu, Meneja Mauzo wa AAR Insurance Tanzania, Bi Tabia Masoud alisema“ni utamaduni wetu kama kampuni kuwajali wateja wetu na jamii iliyotuzunguka kama jinsi tunavyojali familia zetu. Tunafanya hivi ili kuona watu wote katika jamii wakiishi maisha bora.”

“Tunaona fahari kuweza kutoa msaada kwa wazee kwani kundi muhimu katika jamii yetu. Wazee hawa wanaishi katika mazingira magumu, hivyo ni matumaini yetu kwamba msaada huu utaleta utofauti katika maisha yao na kuwawezesha kuendelea kufurahia maisha ipasavyo.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: