Thursday, June 23, 2016

ASILIMIA 89 YA WATANZANIA WAMKUBALI RAIS MAGUFULI, AWAPIKU JK NA LOWASSA; UTAFITI WA CZI WABAINISHA

Mwanasheria msomi, kutoka taasisi huru inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya habari, (CZI), David Saile Manoti, (katikati), akiwa na wasomi wenzake, Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma
---
TAASISI ya ushauri wa mambo ya Habari ijulikanayo kama CZI, imetoa utafiti unaoonyesha kuwa katika kipindi cha miezi 8 ya utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Watanzania wengiwanamkubali Rais na wanayo imani kubwa Tanzania itarudi kwenye “mstari’.

Watafiti hao, ambao ni David Saile Manoti ambaye amebobea kwenye masuala ya Sheria, Juma
George Chikawe, yeye ni mtaalamu wa Teknohama, na Dotto Nyirenda ambaye
amebobea kwenye masuala ya Kidiplomasia, wamesma sambambana utafitihuo pia
wameelezea kuwa Rais Magufuli atakapopewa dhamana ya kukiongoza Chama Cha
Mapinduzi CCM hapo Julai 27 kwenye mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala,
ufanisi wake katika kuongoza nchi utaongezeka.

Kwa mujibu wa wanazuoni hao, walisema utafiti wao ulifanyika nchi nzima na walitumia njia ya kuwahoji watu papo kwa hapo, kuwahoji kwa kupitia simu au kuwahoji kimakundi.

Akizungumzia utafiti wa miezi 8 ya Rais Magufuli akiwa madarakani, Mwanasheria David Saile Manoti, alsiema, kundi la kwanza walilolihoji ni lile la vijana wenye umri kati ya miaka 14-18 ambao wengi wao ni wanafunzi. “Baada ya kundi hili kuhojiwa lilionyesha imani kubwa ya Rais kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi, atarejesha nidhamu ya masomo mashuleni.” Alsiema Manoti.

Kuhusu kundi la vinaja wa miaka 10-30 asilimia 82 ya waliohojiwa wameonyesha imani kuwa Rais John Magufuli ataleta mageuzi kwenye elimu hususan masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kumaliza tatizo la mabweni wka wanafunzi.

Akizungumzia kundi la miaka 30-60, Manoti alisema, Watumishi wa umma wameonyesha imani kuwa Rais Magufuli atarejesha imani kwa serikali kutokana na jinsi anavyoshughulikia
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Aidha utafiti unaonyesha kuwa asilimia 89.0 ya kundi hili limeonyesha imani kubwa kwa Rais kumaliza matatizo ya wazee kwa kuanza kuwalipa posho kwa mwezi.

Katika utafiti huu, Manoti amebainisha kuwa umoja na mshikamano mongoni mwa Watanzania utaimarika zaidi, vile vile kundi hili limesema Rais Magufulu anazidi kuwa maarufu huku wapinzani wakionekana kupoteza umaarufu klutokana na kushindwa kubuni mbinu mpya ya mapambanoya kisiasa. "Kwa ujumla wake Mh. Rais Magufuli anakubalika kwa asilimia 89% huku akiwapiku Edward Lowassa na Mh. Jakaya Kikwete ambao wao wamegawana zilizobaki, Mh. Kikwete asilimia 7% na Mh. Edward Lowassa akiwa na asilimia 4%.

Akizungumzia mkutano mkuu maalum wa CCM, Mwanadiplomasia Dotto Nyirenda yeye amewaasa wana CCM kutambua mambo 10 ambayo Rais Magufuli anatosha kuyasimamia.

Aliyateja mambo hayo kuwa ni pamoja na rasilimali watu, rasilimali ardhi, majengo na viwanja, wanazuoni wa kila taaluma, wafanyabiashara ndogondogo (machinga), wanayabiashara, wanachama wanaozidi milioni 9, Mashabiki wake wanaozidi milioni 28.9, wakulima, wavuvi, na wafugaji, laini pamoja na “utajiri” huo, CCM haiwezi kujiendesha na inategemea ruzuku kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, pamoja na wafadhili ambao wengine sio wasafi kwenye rekodi zao.
Dotto Nyirenda, Mwanadiplomasia, czi
Juma George Chikawe, Mtaalamu wa Teknohama CZI

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu