Monday, June 13, 2016

GSM FOUNDATION WAMEFANYA NA HILI HUKO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema na Meneja Mkuu wa GSM Foundation Shannon Kiwamba wakiwa kwenye stoo ilipohifadhiwa saruji hiyo
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema akizungumza na wazazi juu ya kukabidhiwa, mifuko hiyo 600 ya Saruji katika Shule ya Msingi Mbande leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mkuu wa GSM Foundation Shannon Kiwamba.
Sehemu ya wazazi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbande mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo 600 ya Saruji leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema na Meneja Mkuu wa GSM Foundation Shannon Kiwamba wakikabidhi mifuko hiyo 600 ya Saruji kwenye uongozi wa Shule ya Msingi Mbande leo jijini Dar es Salaam.
---
Na Mwandishi Wetu

Katika kuhakikisha azma yake ya kuchangia kwa kiasi kikubwa uboreshwaji wa sekta za elimu na Afya nchini, Taasisi ya GSM Foundation imemkabidhi mifuko 600 ya saruji kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi Sofia Mjema, ambayo itatumika kuboresha mazingira ya elimu katika Shule ya Msingi Mbande iliyopo kata ya Chamazi ikiwa ni jitihada za kuboresha elimu kwa kukabiliana na changamoto za Uwepo wa madarasa uliokuwa unaikabili shule hiyo kwa muda mrefu.

Akiongea katika kukabidhi madawati hayo, Afisa Mawasiliano wa kampuni ya GSM, Halfan Kiwamba amesema, shehena hiyo ni sehemu tu ya misaada inayotawanywa nchi nzima na taasisi hiyo yenye lengo la kuwekeza kwenye Afya na elimu bora kwa kizazi kijacho.

Kiwamba amesema GSM Foundation ina lengo la kusaidia wananchi, hasa wenye kipato cha chini kuhakikisha kwamba watoto wao wana elimu nzuri na uhakika wa Afya zao ili waweze kujiandaa vema kulitumikia Taifa la kesho.giza kila chumba kukaa wanafunzi 45.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu