Sunday, June 26, 2016

JUMAPILI NJEMA; NENO KWA WOTE WANAO SUBIRI MAJIBU YA MAOMBI YAO TOKA KWA MUNGU

Tembo na mbwa walishika mimba kwa wakati mmoja. miezi mitatu baadae mbwa alizaa watoto sita.

baada ya miezi sita mbwa alibeba tena mimba nyingine, na ilipofika miezi tisa alizaa watoto wengine kumi na wawili

Miezi kumi na nane baadae mbwa aliamua kumfuata tembo na kumuuliza "unahakika kwamba kweli una mimba"? Maana sote tulibeba mimba wakati mmoja, mimi nimeshazaa mara mbili mpaka sasa nina watoto zaidi ya zaidi lakini wewe bado una mimba ileile tu, nini kinaendelea?

Tembo akajibu "kitu kimoja ambacho inakupasa utambue ni kwamba nilie mbeba tumboni mwangu sio mbwa bali ni tembo. AkaendeIea huku akisema ninazaa mara moja tu ndani ya miaka miwili, lakin siku nikimshusha mwanagu ardhini dunia lazima ihisi kitu, na pindi mwanangu anapokatiza barabarani, binadamu husimama na kusitisha shughuli zao hivyo basi nilichobeba kina thamani kubwa sana."

FUNZO
Usipoteze imani yako unapoona watu wengine wanajibiwa maombi yao, wala usivunjike moyo kama bado hujapokea baraka zako toka kwa Bwana.

Sema na moyo wako kwamba"siku yangu ya kupoke Majibu ya maombi yangu inakuja, Amini Bwana hachelewi wala hakawii, punde Bwana atajibu maombi yako na kwa hakika utaishangaza dunia."

Imeletwa kwenu na Mdau Hellen Kwavava,
Dar es Salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu