Monday, June 27, 2016

KUONA YANGA NA TP MAZEMBE NI BURE

 AMINI , USIAMI Ndivyo ilivyo baada ya Uongozi wa timu ya Yanga kutoa ‘ofa’ yaa buree kwa mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu ‘Bongo’ kutimba uwanja wa Taifa Jumanne hii kushuhudia ‘game’ ya Yanga na Tp Mazembe bureee bila kulipia hata shilingi.

Uamuzi huo wa umetolewa leo hi na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuf Manji kwa lengo moja la kuwawezesha mashabiki hao kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ili kuipa sapoti ya nguvu Yanga dhidi ya Mazembe katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho.

Imeelezwa, uamuzi huo umepitishwa usiku huu baada ya viongozi wa Yanga kukutana katika kikao cha pamoja na Mwenyekiti, Yusuf Manji.

"Kikao ni kati ya baadhi ya viongozi pamoja na mwenyekiti. Uamuzi ni kwamba mechi hiyo itakuwa haina kiingilio na mashabiki waaruhusiwa kwenda kwa wingi kuishangilia Yanga," kilieleza chanzo.

"Si lazima kila shabiki anayekuja awe wa Yanga, waambie na mashabiki wa Simba waje. Hata kama watabeba bendera tu za Tanzania.

"Yanga ni ya Tanzania, Yanga haitokei Congo na TP Mazembe haitokei Tanzania, waje waishangilie timu ya Tanzania."

Awali mchezo huo ulipanaagwa kuwa na vingilio tofauti kabla ya kufikiwa kwa uamuzi huo uliopokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka hapa nchini wakiwemo wapinzani wa jadi wa timu ya Yanga (Simba) waliodai kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na hofu ya ubora wa timu ya Mazembe na lundo la mashabiki linaloongozana na timu mahali popote pale ambapo timu yao inasafiri kwa ajili ya mchezo wake.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu