Thursday, June 2, 2016

MSANII DIAMOND PLATINUMZ AMSAINI MSANII RICH MAVOKO KATIKA LEBO YAKE WCB

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akibadilishana mkataba na Rich Mavoko mara baada ya kusaini huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza  amezindua rasmi Lebo ya muziki ‘WCB Record Label’ na kuwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo hiyo huku msanii Rich Mavoko akisaini mkataba wa kufanya kazi na Lebo hiyo ndani ya Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz (wa pili kushoto) akiwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo ya ‘WCB Record Label’ ambayo ameizindua leo ndani ya hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza pamoja na mameneja wake Hamis Tale na Mkubwa Fela. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Msanii Queen Darleen, Raymond na Hamonize.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz (wa pili kushoto) akiwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo ya ‘WCB Record Label’ ambayo ameizindua leo ndani ya hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza pamoja na mameneja wake Hamis Tale na Mkubwa Fela. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Msanii Queen Darleen, Raymond na Hamonize.
---
Lebo ya muziki ‘WCB Record Label’ imezinduliwa rasmi huku msanii Richard 'Rich Mavoko' akisaini mkataba wa kufanya kazi zake za muziki chini ya lebo hiyo inayosimamia wasanii wengine watatu.

WCB inakuwa ni lebo ya kwanza nchini Tanzania kuanzishwa na kusimamiwa na mwanamuziki, ikilinganishwa na lebo kadhaa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na wadau waliokuwa katika tasnia ya sanaa na burudani.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu WCB, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz alisema lengo la kuanzisha lebo hiyo ni kusaidia vijana wenye vipaji na kuifanya sanaa ya muziki izalisha pato la taifa.

Alisema WCB inajaribu kuangalia ni namna gani shughuli za kimuziki zitaweza kusaidia vijana wenye vipaji mtaani kushikamana kwa pamoja ili na wao kufanikiwa kimuziki na kusaidia familia zao.

“Sanaa siyo ulimwengu wa vita ni wasanii kwa wasanii kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuleta sifa kwa nchi na familia zetu zikafanikiwa kiuchumi, tunachokifanya ni kuonyesha upendo baina yetu na sisi wenyewe tukaliletea sifa taifa letu,” alisema Diamond.

Alisema kuna kila haja kupitia muziki kama ilivyo kwa biashara nyingine, ukachangia pato la taifa na kubadili maisha ya vijana walio wengi, lakini pia tutakuwa mfano bora kwa jamii.

Diamond alisema si wanasiasa pekee wanaoweza kubadili maisha ya Watanzania, bali nyanja tofauti kwa nyakati zake wakiwemo wanamuziki wanaweza kufanya mabadiliko katika taifa.

“Serikali ilikuwa imeanza kuunga mkono juhudi za wasanii, lakini inashindwa namna ya kutukusanya na kutusaidia katika umoja wetu itasaidia wao kuona ni namna gani watatufikia lakini pia tutapata riziki ambayo hata serikali itapata mapato kupitia fani ya muziki na sisi tukachangia katika pato hilo la serikali, kama ilivyo kwa biashara zingine ndiyo kwanza tunaanza,” alisema Diamond Platnumz.

Diamond anasema tangu kuanzishwa kwa lebo hiyo, tayari imefanikiwa kuajiri watu 41, ambao wanalipwa kutokana na kazi mbalimbali zinazofanyika katika ofisi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji WCB, Said Fella alisema lebo hiyo ilianza kufanya kazi na wasanii watatu akiwamo Queen Darleen, Harmonize a Raymond na hivi sasa wamesaini mkataba na Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne kujiunga na lebo hiyo.

Alisema wakati anaanza muziki, Diamond alilazimika kutengeneza jila lake kwanza na baadaye alitafuta nembo ‘logo’ ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo kwa hivi sasa imekuwa lebo inayosimamia kazi za wasanii.

“Baada ya kutengeneza jina kaamua kutengeneza logo yake mwenyewe WCB, ameitengeneza jinsi awezavyo na sasa imefikia hatua ameamua kuzindua lebo na imefikia hatua sasa tunaanza kusaidia wasanii awe mkubwa au mdogo lakini kwa sasa tunao watatu, tumeanza kufanya kazi na Harmonize, tukaja Raymond sasa hivi tumemuona Rich Mavoko,” alisema Fella.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu