Sunday, June 26, 2016

MTEMVU ALIA NA HUJUMA ANAZO FANYIWA

Aliyekuwa Mbunge Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), amelalamikia kuhujumiwa baada ya ofisi zake kwa nyakati tofauti kisha kumwibia nyaraka mbalimbali na mali za thamani kubwa.

Matukio hayo yamefanyika kwa nyakati tofauti ambapo Machi 5, mwaka watu wasiojulikana walivunja ofisi yake iliyoko Posta katikati ya Jiji la Dar es Salaam waliiBa vitu mbalimbali wakati tukio kama hilo lilirudiwa Machi 13 katika ofisi yake ya Chang'ombe ambapo zilichukuliwa nyaraka za uchaguzi wa mwaka jana pekee licha ya kuwa kulikuwa na vitu vingine vya thamani kubwa.

Hali kadhalika usiku wa kuamkia Juni, 26 (leo) wezi hao wameingia tena katika ofisi hiyo baada ya kufanikiwa kumpa mlinzi chakula kinachodaiwa kuwekwa dawa za kulevya ambapo alilala ndipo walipata mwanya wa kuiba pikipiki tatu zilizokuwa zimehifadhiwa katika ofisi hiyo, viroba vitatu vya mchele na boksi tano za tende.
Abbas Kilapo (aliye vaa kofia) akiwaonyesha Askari kanzu wa Kituo cha Chang'ombe jinsi watu hao walivyofanikiwa kwa kuondoka na vitu hivyo.
Muhusika wa ofisi hiyo ambaye alifahamika kwa jina la, Abbas Kilapo akiwaonyesha Askari Kanzu na waandishi wa hapari (pichani hawapo) Namba za pikipiki na kadi za Pikipiki zilizoibiwa na watu wanaodaiwa ni wezi.
Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Miburani, Ally Kamtande akimpepea inzi mlinzi huyo Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu