Wednesday, June 29, 2016

MAONI YA MSOMAJI; NAPINGA, NALAANI, NAKEMEA TABIA YA KUKUZA NA KUENEZA TABIA ZA USHOGA NCHINI

Na Martin Maranja Masese.

Sikuwepo nyumbani, ila ilipofika mida ya saa 3 usiku, rafiki yangu mmoja akaandika katika kundi mojawapo la whatsapp, kwamba washa Tv, mtazame kipindi cha Take One cha Clouds Tv... Nikapuuzia.., nikapigiwa simu na jamaa kadhaa, wakinitaka niwashe luninga yangu.., Nikawauliza kuna nini.. wakasema wewe washa uone shoga anahojiwa... Nikahamaki..,

Nilipofika nyumbani.., nakuta watoto wangu, familia yangu imeweka kipindi cha Take One cha Clouds Tv, akihojiwa mtu ambaye ametambulishwa kwamba anajihusisha na tabia ya mapenzi ya jinsia moja yaani Shoga.. Nikasikitika sana... (sikumtambua jina, kwa sababu nilikuta kipindi kipo katikati)

Swali la kwanza kuulizwa nikipokanyaga sebuleni ni... ".., Baba shoga ni nani? na mtu akiwa shoga utamtambua vipi? na ushoga unafanywa na watu gani.. hapa wanaonyesha mtu ambaye ni shoga. "..., nikaishiwa pumzi.. Nikashindwa kutoa jibu..., naomba kuuliza na napenda wamiliki wa kituo cha Clouds Tv wanipe majibu.., hivi mnafahamu namna ambavyo, vyombo vya habari vinaleta madhara hasi au chanya kwenye jamii?? Mnafahamu ni kwa kiasi gani tukio la kumuhoji mwanaume huyo ambaye anajihusisha na vitendo vya kidhalimu vya ushoga limeathiri jamii yetu?? Je, baada ya kumaliza kufanya nae kipindi huyo shoga.. Hamkupata namna ya kujiuliza namna gani sahihi kiwafikie watazamaji bila kuwa na athari kwa jamii??

Mnamo miaka ya 1960., mwanamageuzi, mwanasiasa na mtetezi wa haki za binadamu haswa watu weusi, alikuwa akiitwa Malcom X.., aliwahi kusema maneno yafuatayo..

"...,The media's the most powerful entity on earth. They have the power to make the innocent guilty and to make the guilty innocent, and that's power. Because they control the minds of the masses."

Kwa tafsiri isiyo rasmi sana.. ".., vyombo vya habari ni muungano wenye nguvu katika Dunia. Vinaweza kufanya asiye na makosa akaoneka kakosea na kumfanya mwenye makosa akawa siyo mkosaji, na hiyo ni nguvu. Kwa sababu inaendesha mawazo ya watu."

Hivyo.., kikichofanywa na Clouds Tv.., kinaweza kuwa... Kimefanya uzuri uonekane kuwa ubaya au ubaya uonekane kuwa mzuri., na raia watakuwa wamechagua upande sahihi kwao.. Kila mtu kwa utashi wake.

Je, Mnafikiri kumuita mtu huyo, na kumhoji kwenye kipindi chenu chenye zaidi ya nusu saa.., mmeongeza tatizo kwenye jamii au mmepunguza tatizo.. Kwa Kuzingatia kwamba, yule mtu alikuwa akijisifia na akitoa sifa dhabiti za kuridhika na hali ile.. Hadi kufikia hatua ya kusema anataka apewe ujsuzito kwa njia yoyote...

Naomba kumuuliza mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media group... Je, katika kipindi hicho, watanzania wamejifunza nini?? Je, amewaokoa watanzania wangaoi wasijuinge na ushoga? Au kipindi kimeleta faida ipi chanya kwenye jamii??

Naendelea kuhoji.., naomba meneja wa vipindi wa Clouds Media group au clouds Tv.., anieleze, je, anajua kipindi kile cha take one kinatazamwa na watu wangapi?? anajua impact hasi yake kwenye jamii haswaa baada ya kumalizika kipindi kile?? Je, anajua watu wa rika gani wanatizama kipindi kile?? una wahoji vipi mashoga hadharani, tena bila aibu na mtangazaji anafurahia kabisa?? Tena nasikia.. Huyo punga anausifia ushoga... Unafikiri leo amekomba njemba ngapi kuzipeleka motoni??

Sheria za nchi yetu zinasema nini kuhusu masuala haya?? Je, kanuni na sheria za utangazaji na masharti ya utoaji leseni ya vyombo vya habari nchini inasema nini kuhusu masuala haya ya upotovu wa maadili?? Sheria za nchi hazitambui uwepo wa ushoga nchini.. Kwanini mashoga wapate kuhojiwa hadharani, tena mapema.. Tena kwenye Televisheni ambayo inatizamwa sana, na kundi kubwa la watu??

Serikali yangu inapaswa kuchukua hatua stahiki ili kukomesha vitendo hivi, visijirudie kamwe... (kama serikali iliweza kulifungia gazeti la MAWIO kwa tuhuma za kuandika habari za uchochezi, nategemea CLOUDS TV nao kuwajibishwa kwa kusambaza habari za ushoga kinyume na matakwa ya katiba ya nchi)...

Natumai, sekretarieti ya maudhui ya vipindi vya televisheni na redio ya TCRA itaketi chini na kuja na adhabu nzuri kabisa kwa mujibu wa kanuni, ili iwe fundisho kwa watu na vyombo vingine vyenye tabia kama hiyo... Maana, tabia hii ikiachwaa ienee, italeta shida kubwa sana kwenye jamii... Nakumbuka mauaji ya kimbari ya Rwanda.. Wahusika walitumia matangazo ya redio kusambaza chuki dhidi ya raia... Hadi sasa ni historia... Tuwawajibishe clouds Tv kwa hili bila kuwaonea aibu... Hii ni rai yangu kwa TCRA... ambayo ni mamlaka ya mawasiliano nchini... Naamini, haki itatendeka kwetu sisi tusiopenda mambo hayo ya Sodoma na Gomora..

Nchi za wenzetu... Ambazo wanaupinga ushoga na tabia za kushenzi za namna hiyo kwa vitendo.. Wana sheria kali sana... Tunapaswa kuja na sheria kali na kandamizi dhidi ya vitendo vya kipuuzi vya namna hii...

Nchini Urusi... Ukionyesha ethics (maadili) zozote za ushoga hadharani na ukabainika.. Unafungwa miaka isiyopungua 30 jela kwa kusapoti na kueneza ushoga nchini urusi... Hapa kwetu.. Mnawapigia makofi Clouds Tv... MMfano.., Kombe la Dunia la mpira wa miguu, linafanyika Russia mwaka 2018.., serikali ya Urusi imetangaza wazi.. Kama wewe ni shoga au unajihusisha na mapenzi ya jinsia moja l.. Usikanyage Russia... Maana utaishia jela... Sisi hapa.. Tunasifia na kupiga makofi Clouds Tv kuhoji mashoga, tena saa 2 usiku muda wa chakula cha jioni..

Kukipa kitu uhuru wa kuonekana ndani ya vyombo vya habari, na kuruhusu mtu huyo kujisifia hadharani ni kutoa uhalali, na kuruhusu watu waanze kuona mrengo wa kituo husika cha habari kinaunga mkono vitendo hivyo... media ina impact kubwa ndani ya jamii.., kama unafikiri media ni kitu kidogo, muulize Hosni Mubarak, anafahamu ukubwa na impact ya vyombo vya habari katika uenezi wa habari...

Kwa nilichokiona kwenye televisheni ya Clouds Tv... Na iwapo serikali haitachukua hatua stahiki mapema, sitachelea kusema kwa kujipa imani kabisa kwamba.., Kidogo kidogo.....lakini kwa uhakika mkubwa, ndoa za jinsia moja zinakuja... na tayari nimekwisha kuanza kuwaona watetezi wa mambo hayo nchini.... Hivyo, serikali inapaswa kuondoa dhana hiyo kichwani kwangu, ambayo imeanza kujijenga..

Pamoja na kuuchukia kwangu ushoga na kuunga mkono nchi zilizotunga sheria za kupambana na vitendo hivyo, mambo matatu, kwa nafasi yetu kama waafrika haswaa watanzania tunahitaji kuyarekebisha...

Moja, wakati tunapanga adhabu kali, jitihada pia zifanyike za kusaidia waliojiingiza katika vitendo vya ushoga kujitoa..., ika siyo kwa kuwaita kwenye tekevisheni na kuwahoji hadharani.., Nimewahi kusikia kuwa vitendo vya ushoga vina ‘arosto’ (addiction) kama ilivyo kwa wanaotumia dawa za kulevya.

Ingefaa kwa serikali na taasisi zisizo za kiserikali hususani zile za kidini kuanzisha vituo vya kuwashauri na kuwasaidia waathirika.  Ni muhimu kuwasaidia waathirika kabla ya kuwahukumu kwa sababu wengine waliingia katika tabia hiyo kutokana na vitendo vya unyanyasaji walivyofanyiwa wakiwa wadogo.

Pili, wazazi katika jamii zetu tujitahidi kuwalinda watoto wetu kwa kutoa uangalizi zaidi kwao na kuchukua hatua za tahadhari. Tusiwalaze watoto wadogo wa kiume na wavulana wakubwa, tukague watoto wetu mara kwa mara, tusilaze wageni au ndugu na watoto na muhimu zaidi tusiwatetee watuhumiwa wa ubakaji, ulawiti ndani ya familia hata kwa kuwawekea dhamana.

Na tatu na mwisho, wale marais waliotuonyesha ushujaa wao katika kupinga ushoga hebu sasa waonyeshe uhodari wao pia katika kupambana na changamoto nyingine muhimu zaidi ambazo nazo huathiri raia wa nchi zao huenda kuliko hata huo ushoga ikiwemo ufisadi, ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo na biashara ya dawa za kulevya.

Kama wengi wetu tunavyoamini katika mapokeo, nina hakika tutakiri kuwa tunapinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kutokana na mafundisho ya imani ya dini zetu, Uislam na Ukristo.

Kwa mujibu wa dini zetu hizi mbili, vitendo hivyo ni haramu na vinachukiza mbele za Mwenyezi Mungu. Katika Uislam kwa mfano, vitendo hivyo viko katika fungu la dhambi kubwa na kwenye nchi zinazotekeleza sheria za kiislamu, adhabu ya kufanya mapenzi ya mwanaume kwa mwanaume ni kifo.

Hata hivyo ni bahati mbaya kuwa baadhi ya viongozi wa dini duniani wameamua kunajisi dini kwa kubariki vitendo hivi wakitumia misahafu hii... Na wengine kuwataka wafuasi wao wakubali wanachokiamini wao..

Watetezi wa vitendo vya ushoga wana hoja mbili kubwa moja ikiwepo ya ushoga kuwa ni maumbile na ya pili; ushoga kuwa ni sehemu ya haki za binadamu (ya uhuru wa kuchagua kufanya mapenzi na ampendaye)... Laana hii..

Kuhusu ushoga kuwa ni maumbile, ingawa hakuna utafiti uliotoa majibu yanayoweza kumaliza ubishi, swali ambalo watetezi wa ushoga wanapaswa kutusaidia ni je kuzaliwa na ‘walakini’ katika maumbile kunahalalisha kuingiliana watu wa jinsia moja?

Kuhusu hoja ya haki za binadamu, mimi naamini umefika wakati tusione haya kusema tunakataa ushoga kwa sababu ya imani zetu za dini na kwamba madhali sisi ni wengi, demokrasia ichukue mkondo wake kwa matakwa ya wengi kuheshimiwa.

Ni makosa makubwa kwa nchi za magharibi kutarajia dunia nzima iwe kama wao na ndio maana Rais Yoweri Museveni aliwahi kukaririwa akisema jamii ya Waganda iliyokataa ushoga iachwe ijifunze yenyewe kama imefanya makosa au la maana kama nchi ya Uganda ina haki ya kujitungia sheria zake na ikifika wakati jamii ikaona umuhimu wa kuzibadilisha itafanya hivyo kwa uamuzi huru ya wanajamii.

Ni jambo la kusikitisha kuwa watetezi wa haki za mashoga wanasahau haki za binadamu za walio wengi za uhuru wa kufuata mafundisho ya dini zetu na kufuata maadili ya kifamilia na kijamii. Ushoga kama tabia ‘ambukizi’ unatishia maadili yetu ya kidini.

Kwamba ushoga ni haki za binadamu pia inashangaza na inaelekea mradi wa upanuzi wa maana ya haki za binadamu hautofikia mwisho mpaka kutembea utupu hadharani, mapenzi baina ya ndugu wa damu walioridhiana na hata kujiua zitakapokuwa haki za binadamu... Kisa tu wapate mwanya wa kuhalalisha upuuzi huu.. Kitu cha ajabu ni Waingereza walioleta sheria ya kukataza ulawiti Afrika na leo ndiyo wanaozikana!

Ahsante...

Martin Maranja Masse,
Mwananchi wa kawaida.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu