Wednesday, June 15, 2016

SHILOLE ALIA NA WIMBO WA NUH MZIWANDA ... MAPENZI SI UADUNI???

Ikiwa ni siku chache kijana mpiganaji, Nuh Mziwanda aachie video ya wimbo 'Jike Shupa' ambayo inaelezea jinsi alivyoishi na mpenzi wake wa zamani Shilole, Lakini Mwanamama Shilole ameonyesha kukasirishwa na kazi hiyo.

Shilole baada ya kuona video hiyo, aliandika ujumbe instagram ambao baadae aliutoa:

Wale unaongozana nao wanaweza kuwa mizigo au Baraka. Shukrani za dhati kwani kwenye mashabiki zangu ambao ni baraka na pole sana wasanii wote mnaodhani bado tupo dhama za kutumia mgongo wa mtu mwingine kuweza kutoboa. Kipaji siyo maneno ila ni vitendo. Umemiss mkong’oto?... Sipendagi mwanaume mjinga ndiyo maana umekula mkong’oto wa kutosha… Mshamba usiyejua hata kubadilisha boxer, niweke mbali na maisha yako. 

Nikifungua mdomo wangu utadhalilika Shilole na Nuh Mziwanda waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo Nuh amekuwa alizungumzia mengi yaliyomkuta wakati akiwa kwenye mahusiano na mwanadada huyo, huku Shilole akitaa kuzungumzia kilichotokea. lakini mishe mishe media ili mtafuta Nuh Mziwanda na kuweka wazi kuwa ame pigiwa simu na wasanii wezake wakidai Shilole anawapigia simu na kuwaomba wasirushr hewani (wasipost) kava ya video hiyo wala link yake na kuna msanii mwengine alimpigia simu akiwa mbele yangu huku tukimsikiliza anachokisema na kumuomba afanye hivyo.

Naomba kuuliza watu wazima wenzagu... Mapenzi ni uaduni au????? Ukiachana na mtu ndiyo mnajenga uaduni???

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu