Wednesday, June 15, 2016

TAMBAZA AUCTION MART WASEMA WANAOKAMATA PIKIPIKI NA BAJAJ ZINAZOINGIA MJINI NI MATAPELI

 
MENEJA wa operesheni wa kampuni ya udalali ya Tambaza, Dawa Ally Jumanne, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara yahabari Maelezo jijini Dar es Salaam, Juni 15, 2016. Kampuni hiyo ambayo ni wakala wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam katika ukamataji wa pikipiki zinazoingia mjinibila kibali, inatoa taarifa kwa umma kuwakazi hiyo ya ukamataji pikipiki, na bajaji walisitisha tangu Aprili 27, 2016 kutokana na sababu za kiusalama. 

Hivyo basi inawatahadharisha wananchi kuwa wanaofanya kazi ya ukamatajikwasasa ni matapeli na wala sio Tambaza. Tambaza inasema kuwa zoezi hilo la ukamataji litarejea tena mara baada ya kujipanga upya kiusalama, na taarifa ya wao kusitisha zoezi hilo walizitoa kwaMkurugenzi wa jiji, Mkuu wa mkoawa Dar es Salaam, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na makamanda wa polisi wa mikoa yote ya kipolisi jijini Dar es Salaam (Kinondoni, Ilala na Temeke)na maafisa upelelezi wao wote. (NA K-VIS MEDIA/RASHID ZUBERI)

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu