Tuesday, June 21, 2016

TIGO PESA YATOA FURSA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Mkuu wa Huduma za Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Makumbusho Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Tigo Pesa kutoa fursa za biashara kwa wajasiriamali. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedum na kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

WAJASIRIAMALI wa kidijitali pamoja na wabunifu wa matumizi ya simu Tanzania hivi sasa wanaweza kuleta ufumbuzi zaidi kwa mteja katika soko na kuongeza shughuli zao za kibiashara kupitia jukwaa la huduma za kifedha kwa simu la Tigo Pesa.

Tigo Pesa ambayo inaongoza Tanzania kwa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya simu imefuatilia uhusiano wake wa karibu na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuanzisha programu ambazo zinatoa mwongozo wa hatua kwa hatua kwa wajasiliamali wa kijitali kwa kuiunganisha Tigo Pesa katika matumizi yao. Hatua hiyo inajionesha katika wavuti wa www.tigo.co.tz.

Akizungumza katika mkutano na waandioshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za

Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Tigo imewekeza zaidi ya dola milioni 15 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika kuboresha jukwaa la ngazi ya kimataifa na huduma ili kuendelea kutoa huduma sahihi za uhakika, zinazofikiwa na salama kwa wateja.”

Swanepoel alifafanua:“Jukwaa hilo la kuwanunganisha wateja wa Tigo Pesa na mitandao mingine kwa kiwango kikubwa itapunguza changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo katika kuunganisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika kupokea malipo kutoka kwa wateja wake katika hali isiyo na hitilafu na hivyo kuongeza wigo jumuishi kifedha kote nchini.”

Swanepoel aliongeza kwamba, “Tigo pesa imejikita kuangalia hali na uwezo wa kuwezesha maendeleo ya huduma za ubunifu na kujumuisha bila tatizo mitandao mingine ili kuwapa wateja faida zaidi za huduma ya fedha kwa njia ya simu.”

Itakumbukwa kwamba kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, Tigo Pesa ilikamilisha ushirikiano wake na watoaji wengine wa huduma za fedha kwa njia ya simu na benki nchini kwa kuzifanya huduma hizo kupatikana kwa watu wengi zaidi. Tigo Pesa pia ilizindua kifaa cha wateja kwa Android kwa watumiaji IOS, kwa kuwapatia njia rahisi watumiaji pindi wanapotumia huduma zake.

Mfumo wa kuendesha na kutumia program hii ijulikanayo kama ‘Application Program Interface (API) ni muundo wa maelekezo na viwango vya kufikia mtandao kwa kutumia zana za kompyuta au zana za kimtandao. Ili kuzifikia programu za Tigo Pesa inamaanisha wanafunzi wa vyuo, wajasiriamali wa biashara elektroniki , wabunifu wa vifaa na wataalamu wengine wa teknolojia ya habari wanaweza kuibuka na vifaa au kuwezesha vifaa vilivyopo kwa kuunganisha ufumbuzi wao na Tigo Pesa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu