Habari
Kampuni ya Tigo Tanzania leo  imetangaza ofa mpya ambayo watumiaji wote wa simu ambazo ni bandia  watapata simu halisi kila  watakapotembelea duka la huduma kwa wateja la Tigo kubadilishwa simu hizo.

Mradi huu  unalenga kuwawezesha Watanzania kupata simu halisi kutokana na ukomo wa matumizi ya simu  kwa wale walio na simu feki unafikia  mwisho wake.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuwa  simu zote bandia  na ambazo sio za viwango vinavyokubalika  ambazo ziko katika soko la Tanzania  zitazimwa kuanzia Juni 16 mwaka huu.

Akitangaza ofa hiyo Mkuu wa Vifaa wa Tigo, David Zakaria  alisema kuwa kampeni hiyo ya utambuzi imo katika mkakati wa kampuni katika kuisaidia mikakati ya serikali  pamoja na Watanzania  dhidi ya bidhaa bandia  na hali kadhalika  kukidhi usalama wa mifumo ya malipo ya Tigo Pesa.

Akifafanua kuhusu ofa hiyo kwamba  kimsingi inawalenga  wateja walio na simu bandia
Zakaria alisema, “Tunawataka wateja wetu kutembelea maduka Tigo ya huduma kwa wateja  yaliyopo nchi nzima kuhakiki simu zao na baada ya kuhakiki, wote wataobainika kuwa na simu feki watapata simu halisi aina ya Itel 2100 watakaponunua kifurushi cha 22,000/-.

Zakaria alisema ofa hiyo ni nono kwani kwa kawaida, simu hiyo huwa inauzwa kwa bei ya 30,000/- na sasa itapatikani kwa 22,000/- tu, huku akiongeza kuwa simu hiyo itakuwa na dakika 350 za kupiga simu bure katika mitandao yote, ujumbe wa maneno 1,000 na MB250 za intaneti kila mwezi kwa miezi mitatu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: