Baadhi ya wananchi wa Dar es Salaam wamesema Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inapaswa kutafakari upya kuhusu utoaji wa chakula kwa wagonjwa. Wengine wanaamini kwamba utaratibu huo hautakidhi mahitaji ya kila mgonjwa.

“Kwa mfano mimi nina mgonjwa amefanyiwa upasuaji tumboni na mimi ndiye ninayejua anapenda kula nini,” anasema Mariam Aweso, mkazi wa Mwananyamala, “Muhimbili kutoa chakula kwa wagonjwa wengi naamini watakosa lishe wanayoitaka,” Mariam.

Hospitali hiyo imepanga kuaanza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa wote kwa kushirikiana na kampuni iliyopewa tenda ya kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa.
“Naona wengi watachelewa kupata chakula,” anasema Abdallah Hassan, “pia wengine wanatumia chakula cha familia kugawana na mgonjwa maana vipato vyetu vinatofautiana” Hassan, mkazi wa Makongo.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Bi. Aminiel Aligaesha, amesema mgonjwa aliyelazwa atachangia kiasi cha shilingi 50,000. Mchanganuo wake ni kwamba shilingi 30,000 kwajili ya chakula. shilingi 10,000 ni gharama ya kumuona daktari, shilingi 10,000 ni gharama ya kulazwa. Utaratibu huo unapaswa kuanza Julai Mosi.
Na Magreth Mhuza, Dar es Salaam
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: