Monday, June 6, 2016

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO YAKABIDHI BENDERA YA TAIFA KWA MSHINDI WA AIRTEL TRACE MUSIC STARS

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (kulia), akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star 2016, Melisa John, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika fainali za mashindano ya Afrika zitakazofanyika Lagos nchini Nigeria Juni 11 mwaka huu. Wanaoshuhudi ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza.

---
*Mshindi anaenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika nchini Nigeria

Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imekabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars ambaye ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika inayotegemea kufanyika Lagos Nigeria

Melisa John mwenye umri wa miaka 22 anayetokea mkoa wa Dar es Saalam aliibuka mshindi katika fainali zilizoshirikisha washiriki tano bora walioingia kwenye kinyanganyiro hicho. Melisa ameondoka nchini tarehe 4 Juni 2016 kwaajili ya mandalizi ya awali na mazoezi ya muziki yatakayoshirikisha washiriki wengine 8 kutoka nchi za Afrika ambazo Airtel inayoendesha biashara zake kisha kushiriki kwenye fainali zitakazofanyika 11 Juni 2016

Akiongea wakati wa kukabidhi bendera, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi alisema Sanaa ni Kazi ,ajira na ni bidhaa yenye thamani kubwa. Muziki kama tanzu mojawapo ya Sanaa ina nafasi kubwa katika kubadili maisha ya mtu na nchi kiuchumi endapo itatumika vizuri. ile dhana kuwa kazi ya Muziki ni kuburudisha imepitwa na wakati.Wanamuziki sasa tuingie kazini.

Ninawapongeza Airtel wamelielewa hili na kuamua kuunga mkono Serikali kwakuwa na mpango kabambe wa kuibua vipaji vya Vijana kupitia Sanaa ya Muziki uitwao Airtel Trace Music Stars wenye lengo la kuwawezesha Vijana,wanamuziki chipukizi kushiriki na kufikia ndoto zao, ikiwa pia ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni inayosisitiza Mashirika na Taasisi kushiriki kikamilifu katika kukuza na kuendeleza Sanaa na Wasanii.

“napenda kumpongeza Melisa kwa ushindi huo na kumuhasa kuonyesha nidhamu na kuwa na mwelekeo wa kufikia lengo lake wake wote wa mashindano kwani mashindano haya yanatoa fursa pana zaidi ya ushindi hivyo hii ni nafasi ya pekee sana kwako kuitumia fursa hii ipasavyo na kuhakikisha unajenga mahusiano mazuri ya kudumu, kuongeza wigo mpana wa marafiki na mashabiki na pia kuonyesha uwezo/ talanta yako katika mziki” aliongeza Kihimbi

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “tunajivunia kuanzisha mpango huu kabambe ambao si tu unawawesha vijana kubadili maisha yao bali unawapa nafasi ya kufanya muziki na kuonyesha vipaji vyao nje ya mipaka ya nchi. Tunafurahi kuwawezesha vijana wanamuziki chipukizi kupata nafasi hadimu za kufanya kazi na magwiji wa muziki duniani kama Akon na Keri Hilston hivyo tunaomba watanzania watumie fursa hizi kupitia programu zetu za kijamii chini ya mpango wetu wa Airtel Fursa kujikwamua kimaisha wao pamoja na jamii inayowazunguka.”

Kwa upande wake Melisa John amewashukuru Airtel na Serikali kwa ushirikiano katika kukuza tasnia ya muziki na kuchochea ajira kwa vijana wengi, “nimejipanga vyema kukabiliana na changamoto iliyoko mbele yangu na ninawaahidi kuipeperusha vyema bendera ya nchi yangu.

Napenda kuwaomba mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla kunipigia kura kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno MEL kwenda namba 15594 kura yako ni muhimu na itachangia kunipa ushindi”

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu