Wednesday, July 20, 2016

AIRTEL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI KUBORESHA USAFI DAR ES SALAAM

 Wapili toka kulia ni Katibu tarafa wa Kinondoni Bw, Fortunatus Fulgence Isakafu akipokea mapipa yakukusanyia uchafu kwaajili ya mtaa wa kumbukumbu toka kwa Afisa mazingira wa Airtel Bwana, Ncheye Mazoya ( wa kwanza kulia) toka kushoto wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Mtaa Kumbu kumbu Bw, Shaban Majeshi na Diwani wa Kata ya Kinondoni Bw, Mustafa Muro. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi ya serikali za mtaa huo.
Toka kulia ni Afisa mazingira wa Airtel Bwana, Ncheye Mazoya na Katibu tarafa wa Kinondoni Bw, Fortunatus Fulgence Isakafu wakikabidhi mapipa yakukusanyia uchafu kwaajili ya mtaa wa kumbukumbu kwa Diwani wa Kata ya Kinondoni Bw, Mustafa Muro na Mwenyekiti wa Mtaa Kumbukumbu Bw, Shaban Majeshi. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi ya serikali za mtaa huo.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa msaada wa mapipa 15 ya kukusanya na kutunzia takataka kwa serikali ya mtaa wa kumbukumbu kata ya kinondoni yenye thamani shilingi milioni 3 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za kutunza mazingira ili kuiwezesha jamii kuishi katika mazingira bora yatakayopelekea kuwa na afya bora.

Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano Afisa mazingira wa Airtel Bwana, Ncheye Mazoya alisema “Airtel tunatambua sana jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kutunza na kuweka mazingira ya jamii kuwa safi. kwetu sisi Airtel Tunaamini kwamba ili tuweze kufanya biashara lazima tuwe na mazingira safi na wateja wenye afya bora, na ndio maana leo hii tunaunga mkono harakati za serikali za kuhakikisha swala hili la kufanya usafi kila mahali linaendelea kufanikiwa

“Tunaamini mapipa haya ya kutunzia taka yatasaidia jamii inayotuzunguka hapa kinondoni na kuweka mazingira katika hali ya usafi na kusaidia kuepusha magonjwa ya milipuko ambayo yamekuwa ni changamoto kubwa sana nchini” alieleza Mazoya

Kwa upande wake Katibu tarafa wa Kinondoni Bwn Fortunatus Fulgence Isakafu Aliwapongeza Airtel kwa mchango wao na kuongeza kwamba tarafa yake ina mpango mkakati wa kutekeleza kwa vitendo kampeni ya usafi kwa kuhamasisha jamii kujitolea katika kutunza mazingira yanayowazunguka na kuyaweka kuwa safi wakati wote.

“Airtel msaada wenu umekuja wakati sahihi kwa kuwa zoezi la usafi kwetu sisi ni endelevu, mapipa haya ya kuhifadhi taka yatasaidia sana kupunguza kuzagaa kwa taka kila mahali na kurahisisha ukusanyaji taka kwa ajili ya kuzipeleka sehemu maalum kwa uteketezaji”

Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali kutuunga mkono na kuungana nasi katika kampeni hii kama walivyofanya wenzetu wa Airtel leo. Alimaliza kwa kusema Bwn, Isakafu

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu