Friday, July 22, 2016

AMANA BANK TANZANIA WAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya AMANA, Juma Msabaha akifafanua jambo kwa wanahabari wakati Benki hiyo ikizindua Rasmi Kituo cha Huduma kwa wateja ambacho ni mahsusi kwa kuwasaidia wateja wake kuzifikia na kuzipata Huduma Zao kiurahisi zaidi

Benki ya kwanza ya Kiislam nchini Tanzania Amana benki leo imezindua kituo chake cha huduma kwa wateja ambacho kitakuwa kikiwasaidia wateja wake kuweza kupata taarifa mbalimbali
kuhusu huduma zao kama maulizo kuhusu bidhaa za amana, ATMs, huduma za mitandao (simu banking) na amana banki mtaani n.k.

Kituo hicho kitakuwa kikifanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 4 na watakuwa wanapatikana kwa nambari 0657980000 ambapo Amana Bank ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri kwa sasa wana matawi saba matano yakiwa Dar es salaam, Arusha, Mwanza na wanatarajia kufungua matawi mengine mikoa mingi zaidi ila waliyoipa kipaumbele zaidi ni Zanzibar na Tanga
Akizungumza na waadishi wa habari meneja mfawidhi na huduma kwa wateja Juma Msabaha Amesema kuwa utaratibu wanaotumia kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awe na tin namba ya biashara kuonyesha kuwa ni mlipa kodi pia awe amefanya kazi zaidi ya miaka miwili.

Munir Rajab – mkuu wa idara ya biashara Amana benki amesema kuanzishwa kituo hicho kuna lengo la kuhitaji kuwa karibu na wateja wao huku akitanabaisha kuwa huduma za kibenki huwa zinafanana lakini kinachoweza kuwatofautisha ni ubora wa huduma kwa wateja na kwamba wao wamejipanga vizuri kuingia kwenye ushindani huo ambapo wameamua kuwa mwaka huu ni mwaka wa mawakala kwa sababu wanahitaji kuweza kuwafikia wateja wao mpaka mahali ambapo hakuna matawi na wataweza kutumia huduma za kibenki kupitia mawakala wao.
Mkuu wa biashara wa Bank ya AMANA nchini Tanzania Munir rajab akieleza mambo mbalimbali kwa wanahabari kuhusu huduma hiyo mpya kutoka kwao.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu