Wednesday, July 27, 2016

ASKARI ALIYEHUSIKA NA KIFO CHA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI AFUNGWA JELA MIAKA 15

Ndugu wa Marehemu Daudi Mwangosi mama Mfugale kushoto akitoka mahakama kuu kanda ya Iringa akiwa na furaha baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa leo kwa askari aliyeuwa kufungwa jela miaka 15. Picha zote na MatukiodaimaBlog.
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akiwa katika foleni ya ukaguzi wa polisi
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akifurahi jambo na ndugu yake mzee Marko Mfugale mahakamani hapo leo
Mdogo na marehemu Mwangosi Bw Mecky Mwangosi kulia akisalimiana na Rais wa UTPC Deo Nsokolo kabla ya mahakama kuanza leo
Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Bw Deo Nsokolo akizungumza na wanahabari baada ya hukumu ya kesi ya mauwaji ya Mwangosi
Wanahabari mkoa wa Iringa wakimsikiliza Bw. Nsokolo leo.
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi akizungumza na wanahabari ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa umoja wao. 
---
MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU ) Iringa namba G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi, wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Dkt. Paul Kihwelo, alisema kuwa mshitakiwa amekutwa na hatia hiyo ya kuua bila kukusudia katika shitaka la pili lililosomwa Mahakamani hapo hii leo, baada ya shitaka la kwanza kusomwa na kukutwa hana hatia.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwezi Februari 12, 2015, na kufikia hukumu hiyo ya kumtia hatiani hii leo. Tukio hilo lilitokea 2/9/2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu