Saturday, July 23, 2016

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI APIGWA RISASI JIJINI DAR

Askari mmoja wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyetambulika kwa jina la Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay Kinondoni Jijini Dar es salaam, ameuawa usiku wa jana Julai 22, 2014 kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati akiwa kazini katika eneo la Sayansi Kijitonyama.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime (pichani) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu