Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo bahasha iliyo na majina ya Wilaya mbili zitakaanzo anza utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya seklta za Umma (PS3) Mkoani Kigoma. Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akionesha bahasha hiyo kwa washiriki. Kushoto ni Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.

Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akitangaza majina ya Halmashauri Mbili za Wilaya ambazo zitaanza katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa PS3 mkoani Kigoma. Halmashauri za Uvinza na Buhigwe zilipita.
Washiriki wakiwepo wakuu wa Wilaya wakishangilia kwa uteuzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko akifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akizungumza namna utekelezaji utakavyofanyika. Wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (katikati) na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.
Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya alisema mradi utaanza mara moja utekelezaji wake na kwa kuanzia wataanza na mifumo ya tehama kwa kuangalia hali ya miundombinu na kuiboresha.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Alphonce
Muro akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi Utumishi, Kajura wakati wa mkutano huo.
Washiriki wakiwa katika mkutano huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
---
HALMASHAURI mbili za Uvinza na Buhigwe mkoani Kigoma zimefanikiwa kuchaguliwa kuanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) awamu ya kwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maemdeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Halmashauri hizo zimechaguliwa miongoni mwa halamashauri nane za mkoa huo ambazo zipo katika mpango wa utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa katika mikoa 13 na utazinufaisha halmashauri 93 hadi kukamilika kwake.

Mradi huo wa PS3 ulizinduliwa mkoani Kigoma juzi na kufanya jumla ya mikoa 11 kati ya 13 iwe imeshazindua mradi huo ambapo mikoa mingine ambayo inatarajiwa kuzindua Jumanne ijayo ni Kagera na Rukwa na kufanya halmashauri 22 kati ya 93 kuanza utekelezaji wa mradi kwa awamu ya
kwanza na utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kwa gharama ya dola za kimarekani Milioni 62.

Mradi huo wa PS3 utatekelezwa kwa awamu mbili mkoani Kigoma ambapo awamu ya kwanza inaanza mwezi huu na awamu ya pili itaanza Novemba mwaka huu.

Awamu ya kwanza ya mradi itatekelezwa katika Halmashauri mbili zenye uhitaji zaidikatika sekta za umma.

Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya alisema alisema mradi utaanza mara moja utekelezaji wake na kwa kuanzia wataanza na mifumo ya tehama kwa kuangalia hali ya miundombinu na kuiboresha.

Dk Mbuya alisema kwa mkoa wa Kigoma Halamsahauri ambazo zitaanza kunufaika na mradi huo ni Halmashauri ya Wilaya Uvinza na Buhigwe ambazo watendaji kutoka halamshauri husika wanaanza mafunzo leo ya siku moja na wiki ijayo madiwani wao nao watapatiwa mafunzo maaluma ya namna ya kushiriki katika utekelezaji wa mradi na yatafayika kwa wiki moja mjini Kigoma.

Mradi huo wa PS3 unalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa na tafiti tendaji.

Ushirkiano huo wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.

Aidha Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo aliwataka watendaji katika halmashauri hizo kuufanya mradi huo kuwa endelevu na haitakuwa busara wahisani wakiondoka na kila kitu kinakufa.

“Tukahakikishe kuwa mradi huu unakuwa endelevu na hata wahisani wakimaliza muda wao sisi tuweze kuendelea kwa mafanikio ambayo yatazisaidia halmashauri zetu katika utendaji,”alisema Pallangyo.

Awamu ya pili ambayo itatekelezwa mkoani Kigoma kwa halamashauri sita zilizobaki utafanyika kuanzia mwezi Novemba mwaka huu na utahusisha Halmashauri za Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Halamashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute.

Mradi wa PS3 utatekelezwa katika miakoa 13 ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: