Mwenyekiti wa CCM,anayeng'atuka, Dkt. Jakaya Kikwete, (wapili kulia), akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa chama hicho, kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa mjini Dodoma Julai 23, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho mtarajiwa, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (PICHA NA K-VIS BLOG/Khalfan Said).
Dkt. Magufuli akimpongeza Dkt. Kikwete baada ya hotuba yake

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said.

MKUTANO mkuu wa CCM umeanza mjini Dodoma leo Julai 23, 2016, kwa wajumbe kupokea taarifa za mkutano huo na kusikiliza hotuba ya Mwenyekiti anayeng’atuka Dkt. Jakaya Kikwete.

Katika hotuba yake Dkt. Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho kumuunga mkono Mwenye mtarajiwa kwa kushioriki ipasavyo katika kutoa ada za uanachama, na kukipigania chama.

Wajumbe wanaofikia asilimia 99, wanatarajiwa kupiga kura baadaye leo ambapo miongoni mwa wageni waalikwa ni viongozi wa vyama vya siasa, na mabalozi wa nchi za nje walioko nchini.
Mwenyekiti wa CCM, Mjini Mzee Borafia, akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa mkutano mkuu
Baadhi ya wanadiplomasia
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM, Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza kwenye mkutano huo wakati wa ufunguzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: