Monday, July 4, 2016

KADI ZA VISA ZA BancABC KUPUNGUZA WIZI WA PESA

Mkuu wa Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo wa BancABC, Bi Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kadi ya VISA ya BancABC maalum kwa wateja wao na hata wasio wateja wao. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba
Mkuu wa Masoko wa BancABC, Bi Upendo Nkini, akielezea faida za kadi Mpya ya VISA ya BancABC inayomwezesha mteja kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi kwa kuwa kadi hiyo inalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.

Kadi ya VISA ya BancABC ndio kadi pekee inayohudumia wateja wa huduma za fedha za mitandao ya simu.

BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imekuja na tiba ya kukithiri kwa wizi wa pesa ambao husababishwa na baadhi ya watu kuzunguka na fedha nyingi mifukoni mwao kwani imeanzisha kadi mpya ya Visa ambayo itaweza kujazwa pesa kwa kutumia shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola ya Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo, Bi Joyce Malai alisema kadi hiyo itaweza kutumiwa na wateja walio na wasio na akaunti za BancABC na kwamba itawapunguzia adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri nadani na nje ya nchi na kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao.

Alisema watumiaji wataweza kupata huduma masaa 24, siku saba kwa wiki mahali popote kupitia ATM zaidi ya 400 zenye huduma ya Visa nchini Tanzania ambapo ATM za aina hii zinafikia milioni 1.3 duniani na pia watumiaji wanaweza kufanya miamala kwa watoa huduma zaidi ya 1000 Tanzania na zaidi ya milioni 35 duniani kote.

“Tumepata ushuhuda na mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu ambao wana watoto wanaosoma nje ya nchi kwani wanaweza kuwatumia fedha za kujikimu kila mwezi bila kuingia gharama za ziada,” alisema.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko, Bi Upendo Nkini, faida nyingine za kadi hiyo ni kama vile kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi zaidi, kuthibiti matumizi kwani utatumia kiasi cha fedha kilichoko kwenye kadi pekee na pia kuwa na amani kwani pesa zinakuwa salama kwani kadi inalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.

Alisisitiza kuwa hii ndio kadi pekee ya Visa Tanzania ambayo unaweza kutumia kwa ruzuku tano ambazoni shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola ya Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza na kwamba kadi hiyo, ambayo inaweza kutolewa kwa mtu kama zawadi, inaweza kutolewa nyingine pindi inapoibiwa au kupotea.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu