Thursday, July 14, 2016

KYERWA NA BIHARAMULO KUANZA UTEKELEZAJI AWAMU YA KWANZA YA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA

Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) mkoani Kagera, Abdul Kitula (kulia) akimkabidhi bahasha iliyo na majina ya Halmashauri mbili zilizopitishwa kuanza utekelezaji wa mradi wa PS3, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msole mjini Bukoba leo. Halmashauri Mbili za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo ndizo zimechaguliwa kuanza utekelezaji wa mradi huo.Source:Father Kidevu Blog
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msoleakizisoma Haklamashauri zilizo chaguliwa ambazo ni Wilaya ya Kyerwa na Biharamuloambazo zimeonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kuimarisha mifumo yake kulinganisha na Halmashauri zingine sita za Karagwe, Muleba, Misenyi, Ngara, Bukoba Mji na Bukoba ambazo zitaingia awamu ya pili.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Col (Mstaafu) Shaban Shaban Ilangu Lissu ambaye Wilaya yake imechaguliwa kuanza awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa PS3.
Ofisa kutoka PS3 Soud Abubakar akiwasilisha sifa na vigezo vilivyo tumika kuzipata Halamashauri mbili za awali zilivyo patikana ili ziweze kuanza utekelezaji wa mradi.

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa kutoka Wilaya mbalimbali.
Washiriki wakifuatilia uwasilishajki huo.
Mwakilishi wa Halmashauri ya Mji wa Bukoba, ambaye ni Mchumi Msaidizi, Rahel Mbuta akiwasilisha kazi za makundi ambazo ziliainisha Changamato na maeneo ya uboreshaji. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu