Friday, July 1, 2016

MASHINDANO YA ROLLING STONE YAANZA RASMI JIJINI ARUSHA

TIMU 20 kutoka ndani ya nchi na Nje ya nchi Tatu zilizothibitisha kushiriki mashindano ya Rolling stone zimeanza kuwasili mkoani Arusha kwa ajili ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Iilboru sekondari na Arusha Meru.

Mikoa hiyo ni Simiyu, Mara, Singida, Dodoma, Lindi, Pwani, tanga, Kigoma, Geita, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Dar es Salaam na Arusha ikiwa ni wenyeji na nchi za nje ni Burundi, Kenya Congo na Zanzibar kama nchi.

Akizungumza mjini hapa Mwenyekiti wa Rolling stone Ally Mtumwa alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na wageni kutoka mikoa mbalimbali wameanza kuwasili.

Alisema mpaka sasa kuna mikoa imeanza kuwasili kwa ajili ya mashindano hayo ingawa idadi tuliyoitarajia kwenye mashindano hayo imekuwa pungufu tofauti na mialiko tuliyoitoa.

“Tulialika mikoa yote ya Tanzania na nchi zote za Afrika masharika lakini nchi zilizotoa majibu kwa njia ya barua ni hizo tatu tu huku zilizotoa majibu kwa njia simu ni nying lakini hatuna uhakika nazo kwani mpaka leo hii ambapo timu nyingine zimeanza kuwasili lakini nchi hizo hazijathibitisha kwa maandisha” alisema Mtumwa.

Mtumwa alisema wametoa nembo itakayowakilisha mashindano hayo ya Rollingstone kuwa ni Tembo kwani mnyama huyo ni wa bahati ambae kwa sasa serikali inapinga ujangili wa mnyama huyo.

“Tumemtumia mnyama tembo kwasababu kwenye mashindano haya tunataka kutoa elimu ya kupinga ujangili unaoendelea nchini na kwa nchi jirani hivyo kupitia mashindano haya najua elimu itafika kwa wakati”alisema Mtumwa.

Habari picha na Woinde Shizza - Globu ya jamii Arusha.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu