Monday, July 18, 2016

MRADI WA AIRTEL NA VETA VSOMO WAVUTIA ZAIDI YA VIJANA ELFU 10 KUSOMA KWA SIMU

 Meneja wa Mradi VSOMO toka VETA kipawa Bw, Gosbert Kakiziba (wapili toka kulia) akimuonyesha Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya bw Charles Mwakalila (wakwanza kulia) teknolojia ya masomo ya VETA kwa njia ya simu za Airtel wa VSOMO unavyofanya kazi wakati wa haflya ya kutambulisha kwa vijana huduma hii mkoani Mbeya katika chuo cha VETA mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya Bw, Stratom Mushi na Mkuu wa chuo VETA Kipawa ambae ni Msimamizi wa Mradi huo wa VSOMO Eng, Lucius Luteganya.
 Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya bw, Charles Mwakalila (wakwanza kulia) akibonyeza kitufe cha simu ili kuzindua teknolojia ya masomo ya VETA kwa njia ya simu za Airtel wa VSOMO wakati wa haflya ya uzinduzi iliyofanyika mkoani Mbeya katika chuo cha VETA mwishoni mwa wiki. aliyemshikia simu ni Meneja wa Mradi huo wa VSOMO toka VETA kipawa Bw, Gosbert Kakiziba (wapili toka kulia) na wengine wakishuhudia ni Mkuu wa chuo VETA Kipawa ambae ni Msimamizi wa Mradi huo wa VSOMO Eng, Lucius Luteganya na Mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya Bw, Stratom Mushi.
Picha ya pamoja ya uzinduzi wa Airtel VSOMO ni Afisa elimu wa Mkoa Mbeyabw Charles Mwakalila (katikati) akiwa na waalimu wa VETA pamoja na baadhi ya vijana walijitokeza wakati wa haflya ya kutambulisha kwa vijana huduma hiyo mkoani Mbeya katika chuo cha VETA mwishoni mwa wiki. hii itawewawezesjha vijana kusoma kozi za VETA kwa njia ya mtandao wa Airtel.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakishirikiana na VETA wametambulisha mfumo wa Masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kwa njia ya simu za mkononi mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki hii huku mfumo huo ujulikanao kama Airtel VSOMO yaani VETA SOMO ukiwa tayari umeandikisha vijana zaidi ya elfu kumi tayari kuchagua kusoma kozi mbalimbali za VETA tangu kuzinduliwa kwake mwaka huu mei.

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kutambulisha wa mfumo wa Airtel VSOMO katika Ukumbi wa VETA Mbeya Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA Kipawa Eng, Lucius Luteganya alisema “Airtel na VETA tumeshafanya utambulisho kwa mikoa mingine minne ikiwemo Mwanza, Dodoma, Dar es salaam, Arusha na leo tuko Mbeya. mpaka sasa zaidi ya vijana 150 mkoani Mbeya wameshajiunga na mtandao wa VSOMO ili kuanza kusoma, hii inaonyesha kuwa mfumo huu wa kusoma kwa njia ya simu umekubalika hapa hata kabla hatujafika kuutambulisha”

“ninatoa wito kwenu vijana kujitoa na kuchangamkia FURSA hii inayoletwa kwenu na VETA kupitia mtandao wa Airtel ili muweze kujiajiri kupitia FURSA ya Airtel VSOMO. alisema Eng Luteganya

Kwa Upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Bw, Charles Mwakalila kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Bw Amos Makalla alipongeza Mradi wa Airtel VSOMO na kubainisha kuwa mfumo huo ni Muarobaini wa suluhisho la kusaidia vijana wengi kupata elimu ya ufundi stadi hasa kipindi hiki tunapoekea kwenye Uchumi wa Viwanda kama ulivyo mkakati ya serika ya Jamuhuri wa Muungano Tanzania

“hii ni program nzuri sana tukiwa tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda kama ulivyo mpango mkakati wa serikali, naamini tutahitaji watendaji wengi sana kwaajili ya viwada hivyo wenye ujuzi kutoka VETA. Nakumbuka hivi karibuni Naibu Waziri wa elimu teknojia na Mafunzo ya Ufundi Eng, Stella Manyanya alitoa tamko kwa mkuu wa VETA Mbeya, akisisitiza VETA ihakikishe inasajili wanafunzi mara mbili ya waliopo, hivyo kupitia mradi huu wa Airtel VSOMO wa masomo ya VETA kwa njia ya simu utasaidia sana VETA Mbeya kusajili hata mara nne ya idadi iliyopo”

“naweza kusema Airtel VSOMO ni muarobaini wakupunguza changamoto ya ukosefu wa wataalam na watendaji wenye ujuzi tunapoelekea kwenye uchumi wa Viwanda” alisisitiza Bw, Mwakalila

Nae mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya Bw, Straton Mushi alisema “Mradi wa Airtel VSOMO uko chini ya Airtel FURSA ili kuwasaidia vijana kujisomea kozi za ufundi stadi kama vile ufundi wa pikipiki, ufundi simu, maswala urembo, ufundi wa kuchomelea na aluminium na kujipatia ajira papo kwa hapo, Airtel tutahakikisha huduma hii inawafikia wengi kupitia mtandao wetu ulionea hapa nchini”

Airtel VSOMO nimfumo wa utoaji wa mafunzo ya Ufundi stadi kwa njia ya simu za mkononi uliobuniwa kwa ushirikiano kati Airtel na Mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hivyo kufanya simu ya mkononi kuwa Darasa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu