Tuesday, July 5, 2016

MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA (PS3) WAZINDULIWA MKOANI KIGOMA

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga akizindua mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika mkoa wake wa Kigoma leo. Mradi huo wa miaka mitano unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID)  na utatekelezwa katika mikoa 13 nchini na kushirikisha Halamashauri 93.
 Mkuu wa Mkoa aliwataka watendaji wa Halamashauri hizo kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha mradi unaleta manufaa kwa jamii na mkoa.
 Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini   Samsoni Anga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga, Kiongozi wa Mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
Kiongozi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya akizungumza na kueleza dhumuni la mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga.
 Mwakilishi kutoka Tamisemi, Mrisho Mrisho akizungumza kuhusiana na mradi huo na namna ambavyo serikali imejipanga kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya  Buhigwe, Kanali. Elisha Marco Gaguti, Mkuu wa Wilaya ya  Kakonko    Kanali.Hosea Malonda Ndagala na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Peter Bura.
 Mkuu wa Wilaya Kasulu,  Kanali. Martin Elia Mkisi akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko, wakifuatilia mada katika uzinduzi huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
 Msimamizi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) Dk Conrad Mbuya akiwasilisha mada baada ya kufanyika kwa uzinduzi.
 Dk Gemin Mtei akiwasilisha mada kuhusiana na mikakati ya kufanikisha mradi huo.
 Aloyce Maziku kutoka PS3 akiwasilisha mada kuhusiana na Tafiti Tendaji.
 Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko akifuatilia mada hizo kwa makini.
Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini.
 Mkuu wa Wilaya ya  Buhigwe, Kanali Elisha Marco Gaguti akisikiliza kwa makini.
 Mkuu wa Wilaya ya  Kakonko Kanali Hosea Malonda Ndagala akiwa makini kusikiliza mada zinazowasilishwa.
 Wakuu wa Wilaya na washiriki wengine wakifuatilia mada.
 Benchi la Ufundi la mradi wa PS3 wakiwa kazini.
 Washiriki wakiuliza maswali
 Matiko Machonchoryo akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa.
 Mshauri wa Habari na Mawasiliano katika Mradi wa PS3, Leah Mwainyekule akielezea jambo.
 washiriki wakiwa mkutanoni.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma (wapili kulia) akiagana na Msimamizi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya baada ya uzinduzi. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini,Samsoni Anga.
 Picha za pamoja na makundi mbalimbali.
Picha ya pamoja kati ya viongozi na waratibu wa mradi wa PS3.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu