Wednesday, July 27, 2016

MSHINDI WA NYUMBA ATUA GLOBAL TAYARI KUKABIDHIWA NYUMBA YAKE

Mshindi wa nyumba ya Global, Nelly Mwangosi (katikati) akiwa katika studio za Global TV Online kabla ya kwenda kukabidhiwa nyumba yake. Kulia ni mumewe Karolo Stephen Magani na kushoto na kijana wao, Emmanuel Karolo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Global wakimsikiliza mshindi wa nyumba.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimpongeza mshindi wa nyumba Nelly Mwangosi (wa kwanza kushoto). Katikati ni Karolo Stephen Magani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo James akimpongeza mshindi wa nyumba Nelly Mwangosi.
Shigongo akiwasihi Watanzania kuendelea kusoma magazeti ya Global na kujishindia zawadi mbalimbali zinazotangazwa kama alivyofanya Nelly Mwangosi.
Shigongo akiongea na mtoto wa mshindi wa nyumba, Emmanuel Karolo.
---
MWANAMAMA Nelly Mwangosi, aliyeibuka mshindi wa droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa muda wa miezi sita, leo ametembelea ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mwenge, Bamaga tayari kwenda kukabidhiwa mjengo wake uliopo Salasala.

Nelly ambaye ni mama wa watoto wawili mwenyeji wa mkoani Iringa, aliibuka kidedea katika droo ya mwisho iliyochezeshwa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam Juni 30, mwaka huu na kuhudhuriwa na mamia ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers, ambayo ni Championi, Ijumaa, Risasi, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda.

Nelly ametua Global akiwa ameambatana na mumewe aitwaye Karolo Stephen Magani, mwanaye Emmanuel Karolo, dada zake wawili Sofia Mwangosi na Lusia Mwangosi pamoja na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki tayari kwa zoezi la kukabidhiwa nyumba yake iliyogharimu mamilioni ya shilingi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu