Sunday, July 3, 2016

MSTAHIKI MEYA BONIFACE JACOB AFUTURISHA KINONDONI JIJINI DAR

Na Janet Josiah.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob juzi Julai Mosi amefutulisha,wananchi wa manispaa hiyo wakiwamo wadau na wanasiasa wa vyama vyote,hafla iliyofanyika katika viwanja hivyo.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Mstahiki Meya alisema Manispaa yake ipo imara kuliko inavyotarajiwa pamoja na kuwepo vikwazo vya hapa na pale.

Akifafanua kauli yake,alisema pamoja na serikali kuu kuchukua tozo yote ya majengo ambayo ni zaidi ya sh bilioni 10 ambayo itakusanywa na TRA,tayari manispaa hiyo imeshajipanga kukusanya kiasi hicho kwa njia nyingine.
 "Kama miezi sita sasa tumeweza kufanya vizuri kuliko manispaa zote...hivyo hatutashindwa kukusanya mapato na kuleta maendeleo.

"Sitaki kuwa mnafiki mwezi huu mtulya wa Ramadhan, kuna vikwazo vingi Kama mnavyosikia na kujionea ila tutavishinda kwa uwezo wake Mungu.

Pamoja na hayo Mstahiki Meya alitoa zawadi ya viwanja vitano vilivyopo Mabwepande kama sadaka kwa makundi yenye mahitaji maalum (walemavu,yatima,mashirika ya dini,watoto wanaolelewa katika Ngo's) kama sadaka toka manispaa hiyo vitakavyotolewa kwa utaratibu kuandika barua ya maombi kwa mkurugenzi .

Hata hivyo aliwashukuru wote walifika kushiriki futari na kueleza kwamba ataendelea kula nao katika kipindi cha miaka mitano kama walivyokuwa wakifanya mameya waliopita Londa na Mwenda.
 CUF - Mwakalishi wake katika shida alisema kuwa hata kama serikali imezuia kufanyika mikutano, huo ni uoga wao, wao kama ukawa watafanya.

CCM Mwakalishi alimshukuru mstahiki Meya kwa mwaliko wa masheikh bila ubaguzi.

CHADEMA Mwakilishi alisema hali ya maisha imebadilika sana hata kufanya waislam wafuturu kwa shida na Chadema itaendelea kupiga kelele.
 MBUNGE Mwakalishi wa Kinondoni Mtulia alisema wabunge wa manispaa ya kinondoni wote wanne (ubungo,kawe,kibamba na kinondoni) wanamasikitiko makubwa sana kwa kuwa wametolewa matumaini ya kuwapa maendeleo wananchi waliyoahidi baada ya serikali kuchukua tozo ya majengo ambayo ndiyo chanzo kikubwa.
Sheikh Katimba alisema hii nchi yetu sote ambayo inaendeshwa na demokrasia lakini hawaelewi kwanini kuna ubakwaji wa demokrasia.

"Tunawaomba wakubwa waache wabunge wafanye kazi yao..."alisema

Aliongeza kwamba bajeti ya sasa ime kuwa ngumu na hapo hapo serikali kuzuia mitumba kuingia nchini hali inayosababisha ugumu wa maisha hata wananchi kushindwa kununua nguo za sikukuu kama walivyoshindwa kununua sukari kipindi hiki cha ramadhan.
Sheikh Katimba aliitaka serikali iache kukurupuka katika uamuzi wake na kufuatilia jambo mpaka mwisho.

Alitoa mfano wa kweli ambao alisema unawaumiza waislam wengi na kwa dini yao kupinga wa wenzao kuitwa magaidi hata kuwekwa gerezani bila ya uchunguzi kukamilika na kuwakamata wanaofatilia,.

"Tunaiomba serikali irekebishe hali hii ya sasa kwani wimbo wa amani aukamiliki bila haki...Innah..."

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu