Saturday, July 23, 2016

MWANAMUZIKI KOFFI OLOMIDE AFUKUZWA NCHINI KENYA BAADA YA KUFANYA SHAMBULIO LA KUMPIGA MCHEZA SHOO WAKE

Mwamamuziki wa DR Congo Koffi Olomide amekamatwa kwa kumshambulia mwanamke katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Koffi Olomide amekamatwa jana usiku baada ya kufanya mahojiano ya moja kwa moja na televisheni moja kubwa nchini Kenya, kufuati IGP Joseph Boinnet kuamuru akamatwe.

Igizo hilo la IGP Boinnet linafuatia video iliyosambaa kwenye mitandao ya jamii ikimuonyesha mwanamuziki huyo akimpiga teke mwanamke mmoja alipowasili JKIA.

Msanii huyo nyota wa muziki wa Rumba aliwasili Jijini Nairobi majira ya saa 12 asubuhi kwa ajili ya onyesho lake linalongojewa kwa hamu litakalofanyika Bomas of Kenya leo.
Mwamamuziki wa DR Congo Koffi Olomide akizuiliwa na askari wa uwanja wa ndege wa JKIA wakati akifanya shambulio. Picha kwa hisani ya Kenya Citizen TV
Wacheza show wake.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu