Saturday, July 23, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ACHAGULIWA RASMI KUWA MWENYEKITI WA TANO WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA, KWA KUPATA KURA ZOTE ZA WAJUMBE WALIOSHIRIKI MKUTANO HUO

Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio ziapatazo 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika. Picha na MMG, DODOMA.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti Mpya, Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika
Makamu Mwenyekiti-Zanzibar Dkt Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10,pichani katia anaeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrhamani Kinana akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya Wajumbe wa Mkutano mkuu Maalum wa chama cha CCM mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh William Mkapa akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
Mwenyekiti Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akimkumbatia Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka kumi.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano mkuu maalum wa CCM wakipiga kura kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho ambaye anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.Mkutano huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye anamaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete amekiongoza chama hicho kwa Miaka 10 na leo anawaaga wanachama na wajumbe mbalimbali wa chama cha Mapinduzi jioni ya leo mjini Dodoma.
Wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wakipiga kura.
Wajumbe wameisha piga kura na mabox yakiwa tayari kuhesabiwa na baadae kutolewa majibu
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh Al Hassan Mwinyi akipiga kura ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi jioni ya leo.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Dodoma Convetion Center,uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM ambaye amemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya Wajumbe mkuu wa Mkutano mkuu wa CCM,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa kabla ya matokeo ya kumpata Mwenyekiti wa chama hicho hayajatangazwa rasmi jioni ya leo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu