Thursday, July 28, 2016

TUMZIKA KWA AMANI MZEE JOSEPH SENGA

Taarifa nilizozipata zinadai, kuwa Mpiga picha Mkuu wa Gazeti la TanzaniaDaima, Mzee Joseph Senga amefariki Dunia huko nchini India alikokuwa akitibiwa.

inaelezwa kuwa alishapatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitalini hivyo akaenda hotelini kwa mapumjziko na kujiandaa kwa safari ya kutoka huko Tarehe 5/8/2016 na angefika Tanzania tarehe 6/8/2016. Kwamba leo hii akiwa hotelini alizungumza na mke wake akamwarifu kuwa anaendelea vizuri na anatarajia kuanza safari ya kurejea nyumbani nchini tarehe 5 na angefika tarehe 6 mwezi ujao.

Baadaye aliomba apelekwe bafuni kwa sababu mkono wake mmoja ulikuwa haujiwezi kujikunja kwa sababu ya oparesheni aliyofanyiwa. Aliogeshwa kisha baadaye akaomba apewe chakula na matunda bila kuchanganywa pilipili na akapewa akala.

Alianza kujisikia vibaya baadaye kati ya saa 12 na saa 1 jioni jana, akaomba arudishwe hospitalini. Wakati anafuatwa dereva tax chini ya gorofa mbili alimokuwa akiishi Mwalimu Senga, walirudi wakamkuta hali yake imeanza kubadirika.

Walimuwahisha hospitalini, kwamba kadri wanavyozidi kupunguza umbali ili hospitali alipokuwa akitibiwa ndivyo hali yake ilivyokuwa ikizidi kubadilika.

Walipofika hospitalini, madaktari walimpima na kukuta Mwalimu Joseph Senga amefariki dunia. Mungu acha aitwe Mungu. Mwalimu Joseph Senga, tunakulilia, Mungu akupokee upumuzike kwa amani. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu