Meneja Masoko kampuni ya bima ya afya AAR Insurance Bi. Tabia Masoud akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati akikabidhi vifaa vya usafi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda kama programu yao endelevu ya kusaidia jamii na kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakua safi. Mwisho kulia ni Afisa Afya mkoa wa Dar es salaam, Denis Kanzola na mwisho kulia ni Msimamizi wa Fedha, Geofrey Masiga wa kampuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda akikabidhiwa baadhi ya vifaa mbalimbali vya usafi na Kampuni ya bima ya afya AAR Insurance Tanzania kama sehemu ya mpango wake kusaidia jamii na kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakua safi. Mwisho kulia ni Afisa Afya mkoa wa Dar es salaam Denis Kanzola, na kushoto ni msimamizi wa fedha Geofrey Masiga wa kampuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda akimshukuru Meneja Masoko wa kampuni ya bima AAR Insurance Tanzania Bi Tabia Masoud kwa msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi kama mpango wake kusaidia jamii, Kulia ni Afisa Afya Mkoa wa Dar es salaam Denis Kanzola na mwisho kushoto ni msimamizi wa fedha Geofrey Masiga wa kampuni hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo amepokea msaada wa vifaa vya usafi kutoka kampuni ya bima ya AAR Insurance Tanzania ikiwa ni ni msaada uliolenga kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi.

Ikiwa ni sehemu ya mpango wake kusaidia jamii, kampuni hiyo ya bima ya afya imetoa msaada wa matoroli 5, mabuti , reki , mafyekeo , mafagio , machepe , glovu na magudulia ya takataka 50 ambapo vifaa hivyo vitagawiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa kwa maeneo ambayo yameathirika zaidi na uchafu.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Masoko wa AAR Bi Tabia Masoud alisema msaada huo pia umezingatia mojawapo ya vipaumbele vya serikali iliyopo madarakani ambapo inataka kuboresha utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa takataka.

Alisema kwamba msaad huo umelenga zaidi kutatua tatizo la ukusanyaji na uhifadhi wa takataka katika jiji la Dar es salaam. Tunalenga kuwa na mkakati endelevu wa wa kusaidia kampeni za uhamasishaji, ushiriki wa jamii na kupunguza tatizo la takataka katika jiji la Dar es salaam.

Mordichai aliongeza kwamba utupaji taka ovyo katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam ni tatizo kubwa hivyo upatikanaji wa vifaa kama magudulia ya kukusanyia takataka ni hitaji la haraka kwa wakazi wa maeneo hayo. “Tumedhamiria kusaidia jitihada za serikali kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi na kuhakikisha tunakuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya kampeni hii”, alisema Tabia Masoud.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema: “Kuanzia wakati tunapozalisha takataka mpaka wakati takataka hizo zinatupwa lazima wote tukumbuke kwamba ni jukumu la kila mmoja wetu kuhifadhi taka vizuri. Nawashukuru AAR Insurance Tanzania, kwa kusaidia jitihada zetu za kuwa na Dar es salaam safi.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: