Muanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Asasi ya FEDHA Jafari Selemani akizungumzia changamoto za vijana na watanzania kwaujumla juu ya kutokufikia Uhuru wa kifedha (financial freedom) ikiwemo ukosefu wa elimu ya usimamizi fedha binafsi ambapo inapelekea umasikini wa watanzania wengi, pia alitumia nafasi hiyo kuzindua progranu ya FEDHA KLABU ambayo itakayowapa fursa vijana kupata elimu ya udhibiti fedha binafsi buree kila jumamosi chuoni hapo.
Ni mshauri wa vijana pia ni Meneja Masoko wa Taasisi ya FEDHA Abdalah Kipinga akiongea na wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro ambapo alizungumzia juu ya maisha ya wanavyuo na changamoto zake na jinsi ya kuzikabili.
Mhamasishaji wa vijana Elly David akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro (hawapo pichani) ambapo alizungumza kuhusu siri ya mafanikio kwa vijana na kuwaasa kusimamia ndoto zao lkatika kongamano lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita chuoni hapo
Wanafunzi wa chuo cha kilimanjaro wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo lililowezeshwa na Taasisi ya Fedha mwishoni wa wiki iliyopita.
Baadhi ya washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji katika kongamano hilo lilifnayika mwisho wa wiki iliyopita chuoni hapo Sinza Mapambano jijini Dar es salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: